Nenda kwa yaliyomo

Vilima vya Cherang'any

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ramani ya Kenya ioneshayo miinuko na mabonde

Vilima vya Cherang'any ni safu ya milima iliyopo katika nyanda za juu magharibi mwa Kenya.

Vilima hivyo vina mmojawapo kati ya misitu mikubwa mitano ya Kenya na ni chanzo muhimu cha maji.

Tambarare yake kubwa ya kati imetenganishwa na mwambao wa Mau unaoinuka kuanzia kwenye mpaka na Tanzania mpaka Vilima vya Cherang'any. Mwambao huo unaonesha mwisho wa tambarare inayoinuka kwenye mteremko wa Mlima Elgon. [1]

Vilima vya Cherangany huvuka kaunti tatu: kaunti ya Trans-Nzoia, kaunti ya Elgeyo-Marakwet na kaunti ya West Pokot. Kilele kirefu zaidi katika safu hizo ni mlima Nakugen, chenye urefu wa mita 3530.[2] [3][4] Vilele vingine maarufu vya safu hiyo ni: Mlima Chemnirot (m 3520), Mlima Kameleogon (m 3500), Mlima Chebon (m 3375), Mlima Chepkotet (m 3370), Mlima Karelachgelat (m 3350) na Mlima Sodang (m 3211).

Vilima hivyo ni makazi ya jamii ya wawindaji-wakusanyaji iitwayo Wasengwer.

Jiolojia

[hariri | hariri chanzo]

Vilima vya Cherang'any viliundwa kutokana na mpasuko. Safu hizi huunda ubavu wa magharibi wa bonde la Ufa la Afrika ya Mashariki lianzialo Jibuti kwa upande wa kaskazini hadi Msumbiji kwa upande wa kusini. Vilima vya Cherang'any vinapatikana kwenye mwambao wenye misitu na vimezingirwa na kuta za majabali kwenye pande tatu. Vilima hivyo vimeundwa kwa miamba na madini mbalimbali yakiwemo Chromite yaliyopatikana hapo na wanajiolojia kipindi cha ukoloni.[5][6]

Ekolojia

[hariri | hariri chanzo]

Vilima vya Cherang'any vinasimamiwa na programu ya mazingira ya Umoja wa Mataifa kama mojawapo ya vyanzo muhimu vitano va maji nchini Kenya.[7] Kwa mujibu wa ripoti ya mwisho, iliyoonesha mabadiliko ya misitu katika vilima hivyo kati ya mwaka 2002 na 2003, ilionesha kuwa eneo hilo ni la mwisho kwa kuathirika kwa ukataji miti kati ya maeneo yote yaliyokuwa chini usimamizi. Huku ekari 174.3 zikiwa zimeharibiwa na ukataji miti, hasa katika kaunti za Elgeyo-Marakwet na Pokot Magharibi. Kwa sababu misitu hii ni ya uoto wa asili, ripoti hiyo inapendekeza paangaliwe kwa ukaribu ili kuepusha uharibifu zaidi.[8] Hifadhi hizo kumi na tatu za misitu huitwa Misitu ya vilima vya Cherang'any.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Kenyalogy: Geography - Rift Valley and Highlands". www.kenyalogy.com. Iliwekwa mnamo 2008-03-18.
  2. Paul Clarke (1989). The Mountains of Kenya: A Walker's Guide. Mountain Club of Kenya, 1989. uk. 191. Iliwekwa mnamo 2020-03-02.
  3. "Nakugen - Peakbagger". Iliwekwa mnamo 2020-03-02.
  4. "Nakugen". Petter Bjorstad. 2020-02-07. Iliwekwa mnamo 2020-03-02.
  5. "Mountains>Western Highlands". www.magicalkenya.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2008-06-03. Iliwekwa mnamo 2008-03-18.
  6. Joseph Bindloss, Tom Parkinson & Matt Fletcher (2003). Kenya - Google Book Search. uk. 328. ISBN 9781864503036. Iliwekwa mnamo 2008-03-18.
  7. "- Changes in Forest Cover in Kenya's". www.africanconservation.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo Juni 1, 2007. Iliwekwa mnamo 2008-03-18.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  8. "Changes in forest cover in Kenya's five "water towers" 2000–2003". United Nations Environment Programme (UNEP). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 23 Juni 2006.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)