Uwanja wa michezo wa Mbombela
Uwanja wa michezo wa Mbombela ni uwanja wa michezo wa shirikisho la mpira wa miguu na umoja wa michezo ya raga(rugby) unaopatikana Mbombela, hapo zamani palifahamika kama Nelspruit katika jimbo la Mpumalanga, Afrika Kusini. Ulijengwa kwa ajili ya kombe la Dunia la FIFA la mwaka 2010. Ni moja wapo ya viwanja 10 vilivyotumika kwa michezo ya soka na moja kati ya viwanja 5 vipya vilivyo jengwa kwa ajili ya kombe la dunia la mwaka 2010. Ni uwanja wa nyumbani kwa klabu ya Pumas na unauwezo wa kubeba washabiki 40,929 na wote wakiketi kwenye viti.[1]
Unapatikana kilomita sita(6) magharibi mwa jimbo la Mpumalanga na ndio uwanja mkubwa kuliko vyote katika hilo jimbo. Kiasi cha R1,050-milioni kilitumika kujenga uwanja huu na uwanja ulikuwa tayari kabla ya Juni 2010 na fedha zote zilitolewa na serikali kuu kupitia mapato ya ushuru na hapakuwa na kiasi chochote cha fedha kilichohitajika kutoka halmashauri ya jiji.
Matokeo ya Mashindano
[hariri | hariri chanzo]Kombe la Dunia la FIFA 2010
[hariri | hariri chanzo]Tarehe | Muda (UTC+2) | Timu # 1 | Matokeo | Timu # 2 | Mzunguko | Mahudhurio |
---|---|---|---|---|---|---|
16 Juni 2010 | 13:30 | [[Image:|22x20px|border|Bendera ya Honduras]] Honduras | 0–1 | Chile | Kundi H | 32,664 |
20 Juni 2010 | 16:00 | Italia | 1–1 | New Zealand | Kundi F | 38,229 |
23 Juni 2010 | 20:30 | Australia | 2–1 | Serbia | Kundi D | 37,836 |
25 Juni 2010 | 16:00 | North Korea | 0–3 | Ivory Coast | Kundi G | 34,763 |
Kombe la mataifa Afrika 2013
[hariri | hariri chanzo]Tarehe | Muda (UTC+2) | Timu # 1 | Matokeo | Timu # 2 | Mzunguko | Mahudhurio |
---|---|---|---|---|---|---|
21 Januari 2013 | 17:00 | Zambia | 1–1 | Ethiopia | Kundi C | 15,500 |
21 Januari 2013 | 20:00 | Nigeria | 1–1 | Burkina Faso | Kundi C | 13,500 |
25 Januari 2013 | 17:00 | Zambia | 1–1 | Nigeria | Kundi C | 25,000 |
25 Januari 2013 | 20:00 | Burkina Faso | 4–0 | Ethiopia | Kundi C | 35,000 |
29 Januari 2013 | 19:00 | Zambia | 0–0 | Burkina Faso | Kundi C | 8,000 |
30 Januari 2013 | 18:30 | Togo | 1–1 | Tunisia | Kundi D | 7,500 |
3 Februari 2013 | 18:30 | Burkina Faso | 1–0 (Muda wa ziada) | Togo | Robo fainali | 27,000 |
6 Februari 2013 | 18:30 | Burkina Faso | 1–1 (Muda wa ziada) (3–2 pen.) | Ghana | Nusu fainali | 30,000 |
Mechi ya ufunguzi
[hariri | hariri chanzo]Mnamo tarehe 16 Mei 2010, uwanja ulizinduliwa rasmi kwa mchezo wa kirafiki kati ya timu ya taifa ya Afrika Kusini na timu ya taifa ya Thailand. Afrika Kusini walishinda 4–0, wakiongoza 3–0 katika kipindi cha kwanza.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Mbombela Stadium: the stadiums for the 2010 FIFA World Cup South Africa". FIFA.com. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 26 Agosti 2011. Iliwekwa mnamo 2 Desemba 2011.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help); More than one of|archivedate=
na|archive-date=
specified (help); More than one of|archiveurl=
na|archive-url=
specified (help); Unknown parameter|=
ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mambo ya michezo bado ni mbegu. Je, unajua kitu zaidi kuhusu Uwanja wa michezo wa Mbombela kama historia yake, uenezi au kanuni zake? Labda unaona katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine habari zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |