Nenda kwa yaliyomo

Uhamisho wa Babeli

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
James Tissot, Mateka Kuhama (1896) .

Uhamisho wa Babeli (pia: Utumwa wa Babeli) unamaanisha kipindi cha historia ya Wayahudi ambapo idadi yao kubwa kutoka Ufalme wa Yuda walilazimishwa na Wababuloni kuishi ugenini hasa baada ya Yerusalemu kutekwa na kuangamizwa na mfalme Nebukadreza II.

Wayahudi walipelekwa uhamishoni kwa awamu tatu: 597 KK, 586 KK na 582 KK. Ingawa wengine tena walikimbilia Misri, baadhi waliweza kubaki nchini Yuda.

Uwezekano wa kurudi ulipatikana tena Babuloni yenyewe ilipotekwa na Koreshi Mkuu, mfalme wa Uajemi (539 KK). Huyo aliwaruhusu warudi kwao na kujenga upya hekalu la Yerusalemu.

Hata hivyo waliokubali hawakuwa wengi, nao walirudi vilevile kwa awamu. Kati yao kulikuwa na asilimia ya makuhani na Walawi kuliko kawaida, kutokana na uhusiano wao na ibada hekaluni.

Wayahudi wengine waliona maisha huko Mesopotamia yamekuwa na maendeleo kuliko yale ya awali nchini kwao.

Maana ya kidini

[hariri | hariri chanzo]

Vitabu mbalimbali vya Biblia vinahusika na matukio hayo kama ifuatavyo.

Utabiri wake unapatikana hasa katika kitabu cha Yeremia, lakini pia katika Kitabu cha Ezekieli, bila kusahau Kumbukumbu la Sheria ambamo Musa alihimiza Waisraeli kushika masharti ya Agano la Mlima Sinai ili wapate baraka na kukwepa laana.

Uchungu uliofuata unaelezwa kishairi na Kitabu cha Maombolezo.

Sababu zinafafanuliwa hasa na Vitabu vya Wafalme, Mambo ya Nyakati, Kitabu cha Ezra na Kitabu cha Nehemia.

Vyote vinalaumu dhambi kama chanzo cha maangamizi hayo.

Hata hivyo vinatia tumaini kwa kusisitiza uaminifu wa Mungu ambao ni wa milele.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Ramani

Vitabu

Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Uhamisho wa Babeli kama historia yake au athari wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.