Tolomei, Lucho na mwenzao
Mandhari
Tolomei, Lucho na mwenzao (walifariki Roma, Italia, 160 hivi) ni kati ya mashahidi wa imani ya Kikristo waliouawa katika makao makuu ya Dola la Roma wakati wa dhuluma ya kaisari Antoninus Pius.
Habari zao ziliandikwa na Yustino mfiadini ambaye alisimulia jinsi walivyotambulika kuwa Wakristo kwa sababu ya kulaumu maadili mabovu na uonevu wa hukumu wakauawa kwa amri ya liwali Lollo Urbicus [1].
Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kati ya watakatifu wafiadini.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 19 Oktoba[2].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |