Nenda kwa yaliyomo

Teresa Kim

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Teresa Kim (alizaliwa Myeoncheon, Korea Kusini, 1797Seoul, Korea Kusini, 9 Januari 1840), alikuwa mjane Mkristo wa Kanisa Katoliki aliyefia dini yake (pamoja na Agata Yi) kwa kuchinjwa baada ya mateso mengi kuanzia alipokamatwa mwishoni mwa mwaka 1839.

Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri mwaka 1925, halafu tarehe 6 Mei 1984 Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu pamoja na wafiadini wengine 102 wa Korea, wakiwemo Andrea Kim Taegon na Paulo Chong Hasang.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[1], ila ile ya pamoja ni tarehe 20 Septemba.

Mazingira

[hariri | hariri chanzo]

Mwishoni mwa karne ya 18, Ukristo wa Kikatoliki ulianza kuenea taratibu nchini[2] kwa juhudi za wananchi walei. Mwaka 1836 Korea, nchi ya Kikonfusyo ilipata wamisionari wa kwanza kutoka nje (wanashirika wa Paris Foreign Missions Society)[3].

Chini ya nasaba ya Joseon, Ukristo ulifutwa, tena waamini walidhulumiwa na kuuawa. Waliobaki walipaswa kushika imani yao kwa siri.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. Martyrologium Romanum
  2. Michael Walsh, ed. "Butler's Lives of the Saints" (HarperCollins Publishers: New York, 1991), p. 297.
  3. The Liturgy of the Hours Supplement (New York: Catholic Book Publishing Co., 1992, pp. 17–18.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.