Tawasifu ya Malcolm X

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tawasifu ya Malcolm X
Toleo la Kwanza
MwandishiMalcolm X with Alex Haley
NchiMarekani
LughaKiingereza
AinaTawasifu
Kimechapishwa1965 (Grove Press)
OCLC219493184

Tawasifu ya Malcolm X (kwa Kiingereza: The Autobiography of Malcolm X) kilichapishwa kwa mara ya kwanza mnamo 1965, likiwa tokeo la ushirikiano kati ya mwanaharakati wa haki za binadamu Malcolm X na mwandishi wa habari na mtunzi wa vitabu Alex Haley. Haley alisaidiana kuandika tawasifu hii kwa kulingana na matukio yaliyotokana na mahojiano mazito yaliyofanywa kati ya 1963 hadi 1965 mwaka ambao Malcolm X aliuawa kwa kupigwa risasi mfululizo. Tawasifu inahusu mazungumzo ya kiimani ambayo yanaelezea falsafa ya Malcolm X juu ya fahari ya mtu mweusi, uzalendo wa mtu mweusi, na Umajumui wa Afrika. Baada ya kiongozi kuawa, Haley aliandika hitimisho la kitabu. Ambalo jambo hili walikubaliana kabla umauti haujamfika. Katika hitimisho alielezea namna walivyokuwa wanachakata habari za matukio mbalimbali hadi mwisho wa maisha ya Malcolm X.

Wakati Malcolm X na wasomi ambao wa rika moja na kipindi ambacho kitabu kinachapishwa wanamuona Haley kama mwandishi nyuma ya pazia, wasomi wa siku hizi humuona Haley kama moja kati ya washirika bora kabisa katika uandishi. Wanasema kwa makusudi amezima mamlaka yake kama mwandishi ilimradi tu kutengeneza mahusiano bora kabisa na Malcolm X wakati wa uchakataji, jambo hili limefanya kitabu kionekane kama kinaongea moja kwa moja na wasomi wa kitabu. Vilevile Haley alitia baadhi ya matakwa ya Malcolm X ya kifasihi. Kwa mfano, Malcolm X aliondoka katika jumuia ya Nation of Islam wakati wa kipindi hiki kigumu alikuwa anaandaa kitabu na Haley. Badala ya kuandika mabaya juu ya kitendo walichofanya jumuia ya NOI, Malcolm X kakataa kabisa kuanika habari za NOI, Haley kakubaliana na hilio. Kwa mujibu wa "Manning Marable", "Haley alikuwa na wasiwasi kuhusu mtazamo wa Malcolm X juu ya chuki dhidi ya Wayahudi na kuamua kuandika upya baadhi ya matini yake na kuondoa yale yenye ukakasi wa kibaguzi wa Wayahudi.[1]

Kipindi ambacho Tawasifu hii imechapishwa, mchambuzi wa The New York Times alielezea kitabu kama kitabu kizuri na muhimu kilichoambatana na maumivu makali. Mwaka wa 1967, mwahistoria na profesa John William Ward aliandika ya kwamba kitabu kitakuja kuwa tawasifu bora kabisa ya Kimarekani. Mwaka wa 1998, jarida la Time walikitaja kitabu cha Tawasifu ya Malcolm X kama moja kati ya vitabu 10 vya kweli. James Baldwin na Arnold Perl walichukua kitabu hiki na kukitengenezea filamu; andiko lao la filamu lilimsaidia vilivyo mwongozaji Spike Lee kwa ajili ya kutengeneza filamu yake ya 1992 ya Malcolm X.

Muhtasari wa kitabu[hariri | hariri chanzo]

Kimechapishwa baada ya mwenyewe kufa, kwa jina la The Autobiography of Malcolm X kimetaja maisha ya Malcolm X, aliyezaliwa kwa jina la Malcolm Little (1925–1965), ambaye akaja kuwa mwanaharakati wa haki za binadamu. Kwa kuanza na ujauzito wa mama yake, kitabu kinaelezea maisha ya utotoni ya Malcolm akiwa mjini Michigan, kifo cha baba yake kilichotokea katika mazingira ya kutatanisha, na hali iliyopelekea mama yake kuwehuka na kuishia hospitali ya vichaa bila kutaka na kutiwa katika kitengo cha uchunguzi wa kisaikolojia.[2] Maisha ya ujana wa Little yameelezewa pia akiwa huko Boston na New York City, halkadhalika kujihusisha kwake na jamii za kihalifu. Uhalifu huo ambao ulipelekea kutumikia kifungo cha miaka nane-hadi-kumi jela, kifungo ambacho alitumikia miaka sita na nusu (1946–1952) baada ya kupata msamaha.[3] Kitabu kinaelezea ukasisi wake na mkuu wa jumuia Nation of Islam ndugu Elijah Muhammad (1952–1963) na kuibuka kwake kuwa kama msemaji mkuu taifa wa jumuia hiyo. Kinaelezea kuachia kwake ngazi kwenye jumuia hiyo ya Nation of Islam mnamo Machi 1964, na safari yake ya kwenda hija Makka, ambayo ilipelekea kubadili dhehebu na kuwa Sunni, na safari zake za Afrika.[4] Malcolm X aliuawa mjini New York katika jengo la Audubon Ballroom mnamo mwezi wa Februari 1965, kabla kitabu hakijaisha. Mwandishi mwenzake , mwanahabari Alex Haley, alimuhtasarisha siku za mwisho za maisha ya Malcolm X, na kuelezea kwa kina makubaliano yao, ikiwa pamoja na maoni binafsi ya Haley kuhusu muhusika, kwenye hitimisho la "tawasifu".[5]

Aina[hariri | hariri chanzo]

Utunzi wa kitabu[hariri | hariri chanzo]

Malcolm X akisubiria kuanza kwa mkutano na waandishi wa habari mnamo Machi 26, 1964

Haley aliandika kitabu hiki kwa ushirkiano mkubwa kabisa na Malcolm X',[6] ameandika, kapanga, na kukihariri.[7] Tawasifu inatoka na mahojiano mazito zaidi ya 50 yaliyofanywa kati ya Malcolm X baina ya 1963 hadi kifo chake mwaka 1965.[8] Wawili hawa walikutana kwa mara ya kwanza mwaka 1959, wakati huo Haley aliandika makal kuhusu Nation of Islam kwa ajili ya jarida la Reader's Digest, na vilevile mara ya pili pale Haley alipomuhoji Malcolm X kwa ajili ya jarida la Playboy mnamo mwaka wa 1962.[9]

Mwaka wa 1963 kampuni ya uchapishaji ya Doubleday inamwomba Haley kuandika kitabu kuhusu maisha ya Malcolm X. Mwandishi na mtaalamu wa masuala ya fasihi wa Kimarekani bwana Harold Bloom anaandika, "Wakati Haley anamfuata Malcolm na wazo la kumwandikia kitabu kuhusu maisha yake, Malcolm alimpa sura ya mshangao ..."[10] Haley anarejea kwa kusema, "Ilikuwa moja kati ya mara chache sana kumuona akiwa hana jibu la uhakika."[10] Baada ya Malcolm X kuomba ruhusa kutoka kwa Elijah Muhammad, yeye na Haley wakaanza kazi ya kuandika Tawasifu, mchakato ambao umeanza kwa mahojiano ya msaa-mawili-matatu katika studio ya Haley huko mjini Greenwich Village.[10] Bloom anaandika ya kwamba, "Malcolm alimtilia shaka sana Haley hasa kwa kufuatia uwezo wake wa kati na imani yake ya Kikristo na uhudumu wake katika jeshi la Marekani kwa zaidi ya miaka ishirini."[10]

Wakati wanaanza kuandika Tawasifu hii mwanzoni mwa miaka wa 1963, Haley anavurugwa na tabia ya Malcolm X kuongelea kuhusu Elijah Muhammad na Nation of Islam tu. Haley anamkumbusha kitabu kinatakiwa kiwe kinamhusu Malcolm X, na si Muhammad au the Nation of Islam, oni ambalo lilimkwaza Malcolm X. Haley hatimaye anahamisha lengo na kuanza kumhoji kuhusu mama yake mzazi Malcolm X:[11]

Nikasema, 'Bwana Malcolm, je, waweza niambia jambo lolote kuhusu mama yako?' Na kamwe sintokuja sahau jinsi alivyosimama na kuganda kama vile kikaragosi. Halafu akasema, 'Nakumbuka zile aina ya nguo alizokuwa anavaa. Zilikuwa chakavu na rangi ya kijivu iliyopauka.' Halafu akasonga kidogo. Halafu akasema, 'Nakumbuka namna ambavyo alivyokuwa akiinamia jiko, akaijaribu kutupikia kiasi kidogo tulichokuwanacho.' Na huo ndio ulikuwa mwanzo, usiku huo, wa safari yake. Alizunguka katika sakafu hadi kumekucha.[12]

Japokuwa Haley alikaa nyuma ya pazia katika uandishi wa kitabu hiki, wasomi wa kisasa humtazamia kama mshiriki kiini muhimu ambaye amecheza kama umbo lisiloonekana katika kazi za tungo.[13] Amepunguza sauti yake mwenyewe, na kusaini mkataba ambao utakinza mamlka yake ya kiandishi na kutoa nakala za kitabu kama kilivyoandikwa vilevile bila kubadili maneno.[14]

Mchango wa Haley katika kazi hii unajulikana, na wasomi kadhaa wanajadili namna inavyotakiwa kuelezea.[15] Mara kadhaa Malcolm alimtilia shaka Haley. Usiku mmoja wa manane, Malcolm anampigia simu Haley, nakumini asilimia 75. Awali wakati wanaanza alimwambia anamwaini asilimia 25 tu. Hasa ukizingatia Haley alidumu jeshi la maji, miaka 20, msomi wa Mwafrika-Amerika ambao wengi aliwaona kama mamluki tu. Siku ambayo Haley anaambiwa ya kwamba anamwamini asilimia 75, asubuhi yake hakutaka tena kukumbushia jambo la jana usiku. Tangu hapa, Malcolm alikuwa huru sana kwa Haley. Aliongea mengi hadi yale binafsi ya ndani kabisa. Tena kuna kipindi Malcolm alithubutu hata kumpa Haley shajara binafsi aisome.

Haley alijua namna ya kucheza na akili ya Malcolm, kwanza alikuwa hendi nae pupa. Mara kadhaa kaonekana akija ofisini kwa Haley na hasira, anachochora maneno mengi kwenye vikaratasi. Baadaye Haley anatazama, anaona maneno yaliyoweka kwa msimbo, kwa akuwa anamjua Malcolm staili yake, anayasimbua kwa urahisi. Hili lilikuwa la kawaida sana kwa Malcolm kufanya kuchorachora kwenye karatasi. Ikawa sasa akiingia tu ofisini, anamwekea peni na karatasi aanze kuchorachora huku wakijadiliana mambo mengine. Haley anasema, Malcolm alikuwa na uwezo wa kuongelea jambo jengine tofauti kabisa, huku akichora na kuelezea jambo jengine jengine mbali na lile analongelea. Hii michoro imempa mwanga mwingi sana Haley.

Mazungumzo ya wawili hawa, yalikuwa ya kipekee. Haley kavumilia mengi. Mara nyingi humjia nyakati za jioni akiwa katika mizunguko yake akiwa hoi. Upole na hekima ya Haley, ulifanikisha kitabu kuundwa. Kitabu kinaanzia maisha ya utoto, ukubwa, kujihusisha na uhuni, hasira zake juu ya Wazungu na safari yake ya Makka iliyokuja kubadili maoni yake dhidi ya Wazungu na watu weupe kwa ujumla. Baada ya kwenda Makka alikuta Waarabu wasivyo-waba-guzi na kukutana baadhi ya watu rangi nyengine waliomthamini na kumpa mchango wa kifikra na kiroho kwa kiasi kikubwa. Tangu hapa, alibadili kabisa mawazo yake dhidi ya watu wa weupe na Waafrika wenzie ambao walikuwa Wakristo - hasa wale ambao walikuwa wanajipendekeza kwa Wazungu ili kudhulumu haki ya Waafrika Wamarekani wengine.

Safari yake kwenda Afrika, huko Misri, Ghana, Tanzania, Lebanon, Kuwait, Sudan, Kenya, Ethiopia, Nigeria, Liberia, Algers, Guine, kutaja chache. Huku alipata mawazo na mitazamo mipya kabisa.[16]

Kuchapishwa na mauzo[hariri | hariri chanzo]

Tawasifu ya Malcolm X kwenye shelfu ya vitabu ya Ikulu ya Marekani wakati wa urais wa George W. Bush[17]

Kampuni ya uchapishaji ya nchini Marekani, Doubleday, iliingia mkataba wa kuchapisha kitabu cha The Autobiography of Malcolm X na kulipa malipo ya awali kiasi cha dola $30,000 kwa Malcolm X na Haley mnamo mwaka wa 1963.[18] Mwezi wa Machi 1965, wiki tatu tangu kuuawa kwa Malcolm X, Nelson Doubleday, Jr., akafuta mkataba wake aliongia nao kwa kuhofia usalama wa wafanyakazi wake. Mwaka mmoja baadayae, Grove Press, wakachapisha kitabu.[18][19] Kwa vile The Autobiography of Malcolm X imeuza zaidi nakala zaidi ya mamilioni,[20] Marable anaelezea uamuazi wa Doubleday kama janga kubwa lililowahi kufanywa katika historia nzima ya tasnia ya uchapishaji".[21]

The Autobiography of Malcolm X iliuza vyema tangu kuanza kuchapishwa mwaka 1965.[22] Kwa mujibu wa The New York Times, toleo la vitini limeuza nakala zaidi ya 400,000 mwaka wa 1967 na 800,000 zikauzwa mwaka uliofuatia.[23] Hadi kufikia 1970, tawasifu ilikuwa ishachapishwa mara 18.[24] Mwaka wa 1977, The New York Times imeripoti ya kwamba nakala milioni sita za kitabu zimeuzwa.[20] Kitabu kimepitia ongezeko kubwa la wasomaji na kurudia tena kuwa kitabu kilichouza sana kwa miaka ya 1990, kimesaidia sana hasa kwa Spike Lee baada ya kutoa filamu yake 1992 Malcolm X.[25] Between 1989 and 1992, sales of the book increased by 300%.[26]

Maigizo[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 1968, mtayarishaji wa filamu Marvin Worth anamkodisha mtunzi wa riwaya James Baldwin kaundika igizo linalotokana na The Autobiography of Malcolm X; Baldwin aliungana na mwandishi muswaada andishi bwana Arnold Perl, ambaye amefariki mwaka wa 1971 kabla hata hilo andiko halijaisha.[27][28] Baldwin ametengeneza kazi yake ya Tawasifu hii kwa kufuata mfano wa kitabu cha One Day, When I Was Lost: A Scenario Based kwa Alex Haley, kimechapishwa 1972.[29] Waandishi wengine waliojaribu kuandika rasimu ya muswaada huo ni pamoja na mwandishi wa tamthilia David Mamet, mwandishi wa riwaya David Bradley, mwandishi Charles Fuller, na mwandishi-muswaada Calder Willingham.[28][30] Kwa kuongeza filamu, mwongozaji Spike Lee alipitia upya muswaada wa Baldwin-Perl kwa ajili ya filamu yake ya mwaka wa 1992 Malcolm X.[28]

Sura zilizotolewa[hariri | hariri chanzo]

Mwaka wa 1992, mwanasheria Gregory Reed alinunua muswada halisi wa Tawasifu ya Malcolm X kwa kiasi cha dola za Kimarekani zipatazo $100,000 katika mauzo ya Haley Estate.[18] Muswada una sura tatu ambazo hazikuingizwa kwenye kitabu, zinaitwa "The Negro", "The End of Christianity", na "Twenty Million Black Muslims", sura hizo zote ziliondolewa kutoka katika matini halisi ya kitabu.[31][32] Mwaka wa 1964, barua kwenda kwa mchapishaji wake, Haley ameelezea ya kwamba sura hizo kuwa zenye mgongano au hisia kali sana kutoka katika kitabu, baadhi yake zipo kama lava vile moto unawaka".[18] Tofauti kabisa na mawazo ya mwanatawasifu Manning Marable, anaandika ya kwamba, kurasa zilizotolewa zilifanyiwa udikteta kutolewa kwake lakini zilitimia kwa kila hali hasa ukifuatia ziliandikwa kipindi cha miezi ya mwisho-mwisho kabisa ambayo Malcolm X anaondoka katika jumuia ya Nation of Islam.[18]Kwa wao, Marable anasema, Malcolm X alipendekeza kuanzishwa kwa umoja na mshikamano wa Wamarekani Weusi na asasi za kisiasa. Marable anashangazwa na mpango huu huenda ikawa ndio sababu iliyopelekea Nation of Islam na Federal Bureau of Investigation kumnyamazisha Malcolm X.[33] Mwezi wa Aprili 2010, gazeti la New York Post liliripoti ya kwamba kurasa zilizokosekana kwenye kitabu zitachapishwa mbele kabisa na binti wa Malcolm X, Ilyasah Shabazz.[34]

Matoleo[hariri | hariri chanzo]

Kitabu hiki kimechapishwa zaidi ya mara 45 tena katika matoleo ya lugha mbalimbali ikiwa ni pamojaKiabu, Kijerumani, Kifaransa, Kiindonesia. Important editions include:[35]

  • X, Malcolm; Haley, Alex (1965). The Autobiography of Malcolm X (1st paperback ed.). Random House. ISBN 978-0-394-17122-7. 
  • X, Malcolm; Haley, Alex (1973). The Autobiography of Malcolm X (paperback ed.). Penguin Books. ISBN 978-0-14-002824-9. 
  • X, Malcolm; Haley, Alex (1977). The Autobiography of Malcolm X (mass market paperback ed.). Ballantine Books. ISBN 978-0-345-27139-6. 
  • X, Malcolm; Haley, Alex (1992). The Autobiography of Malcolm X (audio cassettes ed.). Simon & Schuster. ISBN 978-0-671-79366-1. 

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Marable, Manning (2005). "Rediscovering Malcolm's Life: A Historian's Adventures in Living History". Souls 7 (1): 33. doi:10.1080/10999940590910023. Retrieved February 25, 2015. 
  2. Dyson 1996, pp. 4–5.
  3. Carson 1995, p. 99.
  4. Dyson 1996, pp. 6–13.
  5. Als, Hilton, "Philosopher or Dog?", in Wood 1992, p. 91; Wideman, John Edgar, "Malcolm X: The Art of Autobiography", in Wood 1992, pp. 104–5.
  6. Stone 1982, pp. 24, 233, 247, 262–264.
  7. Gallen 1995, pp. 243–244.
  8. Wideman, "Malcolm X", in Wood 1992, pp. 103–110; Rampersad, "The Color of His Eyes", in Wood 1992, pp. 119, 127–128.
  9. X & Haley 1965, p. 391.
  10. 10.0 10.1 10.2 10.3 Bloom 2008, p. 12
  11. X & Haley 1965, p. 392.
  12. The Time Has Come (1964–1966). Eyes on the Prize: America's Civil Rights Movement 1954–1985, American Experience. PBS. Jalada kutoka ya awali juu ya April 23, 2010. Iliwekwa mnamo March 7, 2011.
  13. Leak, Jeffery B., "Malcolm X and black masculinity in process", in Terrill 2010, pp. 52–55; Wideman, "Malcolm X", in Wood 1992, pp. 104–110, 119.
  14. Wideman, "Malcolm X", in Wood 1992, pp. 103–116.
  15. Terrill, Robert E., "Introduction" in, Terrill 2010, pp. 3–4, Gillespie, "Autobiography and Identity", in Terrill 2010, pp. 26–36; Norman, Brian, "Bringing Malcolm X to Hollywood", in Terrill 2010, pp. 43; Leak, "Malcolm X and black masculinity in process", in Terrill 2010, pp. 52–55
  16. Malcolm X Travels to Africa and Gain New Insights Archived 15 Desemba 2016 at the Wayback Machine. AfricaResources, 05 May 2007.
  17. Kellogg, Carolyn (February 19, 2010). White House Library's 'Socialist' Books Were Jackie Kennedy's. Los Angeles Times. Iliwekwa mnamo July 11, 2010.
  18. 18.0 18.1 18.2 18.3 18.4 Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named MARABLE312
  19. Remnick, David (April 25, 2011). This American Life: The Making and Remaking of Malcolm X. The New Yorker. Iliwekwa mnamo April 27, 2011.
  20. 20.0 20.1 Pace, Eric (February 2, 1992). Alex Haley, 70, Author of 'Roots,' Dies. The New York Times. Iliwekwa mnamo June 2, 2010.
  21. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named MMAG
  22. Seymour, Gene (November 15, 1992). What Took So Long?. Newsday. Jalada kutoka ya awali juu ya 2012-01-11. Iliwekwa mnamo June 2, 2010. Kigezo:Subscription
  23. Watkins, Mel (February 16, 1969). Black Is Marketable. The New York Times. Iliwekwa mnamo June 1, 2010. Kigezo:Subscription
  24. Rickford, Russell J. (2003). Betty Shabazz: A Remarkable Story of Survival and Faith Before and After Malcolm X. Naperville, Ill.: Sourcebooks. p. 335. ISBN 978-1-4022-0171-4. 
  25. Dyson 1996, p. 144
  26. The Legacy of Malcolm X. U.S. News & World Report (November 15, 1992). Jalada kutoka ya awali juu ya January 14, 2012. Iliwekwa mnamo June 2, 2010.
  27. Rule, Sheila (November 15, 1992). Malcolm X: The Facts, the Fictions, the Film. The New York Times. Iliwekwa mnamo May 31, 2010.
  28. 28.0 28.1 28.2 Weintraub, Bernard (November 23, 1992). A Movie Producer Remembers the Human Side of Malcolm X. The New York Times. Iliwekwa mnamo May 31, 2010.
  29. Field, Douglas (2009). A Historical Guide to James Baldwin. New York: Oxford University Press. pp. 52, 242. ISBN 978-0-19-536653-2. Retrieved October 16, 2010. 
  30. Ansen, David (August 26, 1991). The Battle for Malcolm X. Newsweek. Iliwekwa mnamo May 31, 2010.
  31. Marable & Aidi 2009, p. 315.
  32. Cunningham, Jennifer H. (May 20, 2010). Lost chapters from Malcolm X memoirs revealed. The Grio. Iliwekwa mnamo March 28, 2016.
  33. Marable & Aidi 2009, p. 313.
  34. Malcolm X's Daughter to Add to Father's Autobiography. New York Post (April 12, 2010). Jalada kutoka ya awali juu ya 2013-02-04. Iliwekwa mnamo May 31, 2010.
  35. The Autobiography of Malcolm X: As Told to Alex Haley>editions. Goodreads. Iliwekwa mnamo March 7, 2010.

Vyanzo[hariri | hariri chanzo]

  • Andrews, William, ed. (1992). African-American Autobiography: A Collection of Critical Essays (Paperback ed.). Englewood Cliffs, N.J.: Prentice Hall. ISBN 978-0-13-019845-7. 
  • Bloom, Harold (2008). Bloom's Guides: Alex Haley's The Autobiography of Malcolm X (Hardcover ed.). New York: Chelsea House Pub. ISBN 978-0-7910-9832-5. 
  • Davidson, D.; Samudio, J., eds. (1966). Book Review Digest (61st ed.). New York: H.W. Wilson. 
  • Greetham, David, ed. (1997). The Margins of the Text (Editorial Theory and Literary Criticism) (Hardcover ed.). Ann Arbor, Mich.: University of Michigan Press. ISBN 978-0-472-10667-7. 
  • Marable, Manning; Aidi, Hishaam (, eds. (2009). Black Routes to Islam (Hardcover ed.). New York: Palgrave Macmillan. ISBN 978-1-4039-8400-5. 
  • Wood, Joe, ed. (1992). Malcolm X: In Our Own Image (1st ed.). New York: St Martins Press. ISBN 978-0-312-06609-3. 
  • X, Malcolm; Haley, Alex (1965). The Autobiography of Malcolm X (1st ed.). New York: Grove Press. OCLC 219493184. 

Jisomee zaidi[hariri | hariri chanzo]

  • T'Shaka, Oba (1983). The Political Legacy of Malcolm X. Richmond, Calif.: Pan Afrikan Publications. ISBN 978-1-878557-01-8. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Jua habari zaidi kuhusu Malcolm X kwa kutafuta kupitia mradi wa Wikipedia Sister
Uchambuzi wa kamusi kutoka Wikamusi
Vitabu kutoka Wikitabu
Dondoo kutoka Wikidondoa
Matini za vyanzo kutoka Wikichanzo
Picha na media kutoka Commons
Habari kutoka Wikihabari
Vyanzo vya elimu kutoka Wikichuo
  • Malcolm, website on the life and legacy of Malcolm X