Nenda kwa yaliyomo

Fahari ya mtu mweusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Fahari ya mtu mweusi (kwa Kiingereza: Black pride) ni jina la harakati zilizoanzishwa kuzipiku tamaduni na itikadi za Kizungu na kuhamasisha watu weusi kufurahia tamaduni zao za asili na kushikilia urithi wao wa Kiafrika.[1]

Huko nchini Marekani, harakati hizo zilihusishwa moja kwa moja na kupinga ubaguzi wa rangi kutoka kwa watu weupe. Hasa katika kipindi cha Vuguvugu la haki za kiraia lililotokea nchini Marekani wakati watu weusi walipodai haki zao za kiraia ikiwa ni pamoja na kupiga kura, usawa katika fursa za kazi, sheria za kibaguzi, na mambo mengine mengi ambayo ni haki ya msingi ya kila binadamu.[2]

Harakati nyingine zinazohusiana ni pamoja na mamlaka ya mtu mweusi,[2] uzalendo wa mtu mweusi,[2] Black Panthers na Uafrocentriki.

  1. Lois Tyson (2001). Learning for a Diverse World: Using Critical Theory to Read and Write about Literature. Psychology Press. ku. 208–209. ISBN 978-0-8153-3774-4. Because the dominant white culture in America treated African Americans as subalterns rather than full American citizens and full human beings, the Black Pride movement encouraged black Americans to look to Africa for their cultural origins.
  2. 2.0 2.1 2.2 Wayne C. Glasker (1 Juni 2009). Black Students in the Ivory Tower: African American Student Activism at the University of Pennsylvania, 1967-1990. Univ of Massachusetts Press. uk. 28. ISBN 1-55849-756-0. In 1966 the Black Power-black nationalist-black pride movements emerged as equal and opposite reactions to white racism as a reaction of the biracial civil rights movement.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  • Yúdice, George (1994), "The Funkification of Rio", katika Ross, Andrew; Rose, Tricia (whr.), Microphone Fiends: Youth Music and Youth Culture, London: Routledge, ku. 193–220, ISBN 978-0-415-90907-5