Nenda kwa yaliyomo

Nzi mweleaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Syrphidae)
Nzi mweleaji
Bango la nzi weleaji (spishi za picha 5 na 7 tu zinatokea Afrika ya Mashariki
Bango la nzi weleaji (spishi za picha 5 na 7 tu zinatokea Afrika ya Mashariki
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Diptera (Wadudu wenye mabawa mawili tu)
Nusuoda: Brachycera (Diptera wenye vipapasio vifupi)
Familia ya juu: Syrphoidea
Familia: Syrphidae
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Nusufamilia 4:

Nzi weleaji (kutoka kwa Kiing. hoverflies) ni nzi wa familia Syrphidae katika oda Diptera wanaojulikana kwa tabia yao ya kuelea angani. Spishi nyingi huiga nyigu au nyuki kwa rangi zao mara nyingi kali sana. Nzi-nyuki huelea pia, lakini hawa wana nywele nyingi kwa kawaida.

Urefu wa nzi weleaji huanzia mm 3 hadi 21[1][2]. Umbo lao hutofautiana kutoka kwa mrefu na mwembamba hadi mkubwa na mwenye nywele nyingi. Spishi nyingi zina madoa na/au milia ya rangi kali kama njano, nyekundu au kahawianyekundu. Hata hivyo, wengine ni takriban kabisa nyeusi, kahawia au hata kijani[3]. Baadhi ya rangi husababishwa na akisiko la mwanga na kubadilika kulingana na pembe ya mwanga. Spishi zenye rangi kali hufanana na nyigu au nyuki na hujaribu kuwadanganya mbuai kwa njia hiyo. Hii inaitwa uigizo (mimicry).

Isipokuwa wachache[4], nzi weleaji wanatofautishwa na inzi wengine kwa kuwa na vena bandia ulio sambamba na vena yao ya nne ya kingoringori ya mabawa[1]. Porini, hii ni ngumu kuonwa na huko wanatambuliwa kwa urahisi zaidi na tabia yao ya kuelea. Hata hivyo, hawaelei wakati wa kujilisha. Hiyo ni njia rahisi ya kuwatofautisha na nzi-nyuki, ambao kwa kweli huelea wakati wa kujilisha, isipokuwa kwa idadi ndogo ya spishi, na pia huiga nyuki. Kwa njia nyinginezo za kutofautisha makundi haya mawili ya nzi, angalia makala kuhusu nzi-nyuki.

Wapevu hujilisha kwa mbochi na chavua[3]. Mabuu, kwa upande mwingine, hula vyakula mbalimbali. Baadhi hujilisha kwa dutu ya mimea au wanyama zinazooza, huku wengine hula vidukari, tiripsi na wadudu wengine wanaonyonya mimea[1][5]. Spishi mbuai hufaidia wakulima na watunza bustani, kwani vidukari huharibu mazao, na mabuu wa nzi weleaji hutumiwa mara nyingi katika udhibiti wa kibiolojia. Hii ni pamoja na mojawapo ya spishi zinazoenea sana za nzi weleaji, Episyrphus balteatus, ambaye mabuu yake hula vidukari. Spishi fulani, kama vile Merodon equestris au Eumerus tuberculatus, zinawajibika kwa uchavushaji.

Mabuu ya spishi fulani huishi majini, kama vile mabuu ya Eristalis tenax. Wana neli ya kupumulia kwenye ncha yao ya nyuma na kwa sababu ya hiyo huitwa mabuu wenye mkia wa panya[1]. Huishi katika maji yaliyotuama, hata maji taka[6]. Mara kwa mara wanaweza kuendelea kuishi ndani ya matumbo baada ya kumezwa kwa bahati mbaya na kusababisha shida kidogo kabla ya kutolewa nje[7].

Spishi kadhaa za Afrika ya Mashriki

[hariri | hariri chanzo]
  • Afrosyrphus varipes
  • Allobaccha marginata
  • Allobaccha picta
  • Allograpta calopus
  • Allograpta varipes
  • Asarkina africana
  • Asarkina gemmata
  • Betasyrphus claripennis
  • Betasyrphus hirticeps
  • Ceriana gloriosa
  • Chrysogaster poecilops
  • Episyrphus trisectus
  • Eristalinus aeneus
  • Eristalinus euzonus
  • Eristalinus megacephalus
  • Eristalinus smaragdinus
  • Eristalis tenax
  • Eumerus erythrocerus
  • Eumerus serratus
  • Eupeodes corollae
  • Graptomyza nigricavum
  • Graptomyza suavissima
  • Hovaxylota vulcana
  • Mallota aperta
  • Melanostoma alticola
  • Melanostoma floripeta
  • Melanostoma scalare
  • Mesembrius africanus
  • Mesembrius lagopus
  • Microdon luteiventris
  • Microdon rugosus
  • Ornidia obesa
  • Paragus capricomi
  • Paragus punctatus
  • Phytomia bulligera
  • Phytomia incisa
  • Rhingia cyanoprora
  • Rhingia pycnosoma
  • Senaspis dentipes
  • Senaspis xanthorrhoea
  • Simoides crassipes
  • Sphaerophoria retrocurva
  • Syritta carbonaria
  • Syritta flaviventris
  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 "Hover fly". Encyclopædia Britannica Online. 2009. https://www.britannica.com/EBchecked/topic/273341/hover-fly.
  2. Stubbs, Alan E.; Falk, Steven J (1983). British Hoverflies: An Illustrated Identification Guide (tol. la 2nd). London: British Entomological and Natural History Society. ku. 253, xvpp. ISBN 1-899935-03-7.
  3. 3.0 3.1 "Hoverfly". Hutchinson Encyclopedia. Helicon Publishing. 2009. Archived from the original on 2012-03-08. https://web.archive.org/web/20120308162845/http://encyclopedia.farlex.com/Hover+Fly. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2012-03-08. Iliwekwa mnamo 2022-09-30.
  4. Reemer, Menno (2008). "Surimyia, a new genus of Microdontinae, with notes on Paragodon Thompson, 1969 (Diptera, Syrphidae)" (PDF). Zoologische Mededelingen. 82: 177–188.
  5. Schmidt, Martin; Thewes, Ulrich; Thies, Carsten; Tscharntke, Teja (2004). "Aphid suppression in mulched cereals". Entomologia Experimentalis et Applicata. 113 (2): 87–93. doi:10.1111/j.0013-8703.2004.00205.x. S2CID 85070615.
  6. Aguilera A, Cid A, Regueiro BJ, Prieto JM, Noya M (Septemba 1999). "Intestinal myiasis caused by Eristalis tenax". Journal of Clinical Microbiology. 37 (9): 3082. doi:10.1128/JCM.37.9.3082-3082.1999. PMC 85471. PMID 10475752.{{cite journal}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  7. Whish-Wilson PB (2000). "A possible case of intestinal myiasis due to Eristalis tenax". The Medical Journal of Australia. 173 (11–12): 652. doi:10.5694/j.1326-5377.2000.tb139374.x. PMID 11379520. S2CID 12898612.