Nenda kwa yaliyomo

Stella Damasus

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Stella Damasus (alizaliwa mnamo tarehe 24 Aprili 1978)[1] ni mwimbaji na mcheza filamu kutoka Nigeria.[2] Aliteuliwa kushiriki katika tuzo za Africa Movie Academy Awards za mwaka 2009 katika kipengele cha mwigizaji bora wa kike. Alishinda tuzo ya mwigizaji bora wa kike nchini Nigeria mwaka 2007[3] mnamo mwaka 2012 alishinda tuzo ya mwigizaji bora wa filamu ya Two Brides and a Baby katika tuzo zilizotolewa huko Houston, Texas.

Maisha ya mwanzo

[hariri | hariri chanzo]

Stella Damasus alizaliwa jiji la Benin, jimbo la Edo nchini Nigeria. Ana dada wanne. Alikulia jijini Benin ambapo ndipo aliposoma elimu yake ya msingi.[4] Akiwa na umri wa miaka 13, Stella alihamia Asaba katika jimbo la Delta pamoja na familia yake, huko alihitimisha elimu yake ya sekondari.[5]

Maisha binafsi

[hariri | hariri chanzo]

Damasus aliolewa na Jaiye Aboderin mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 21. Wawili hao walifanikiwa kupata mabinti wawili, kabla ya Jaiye Aboderin kuaga dunia mwaka 2004. Damasus aliolewa tena mwaka 2007 na Bwana Emeka Nzeribe. Ndoa hiyo ilidumu kwa miezi saba kabla ya wawili hao kukubali kutalakiana. Mwaka 2011, alianza mahusiano na mtayarishaji na mwongozaji filamu wa Nigeria Daniel Ademinokan; wamekua katika mahusiano toka hapo hadi sasa. Mahusiano hayo yalileta utata nchini Nigeria pamoja na Afrika kwa sababu hakuna aliekubali wazi kua wapo katika mahusiano hadi ilipofika mwaka 2014.[6]

Damasus alianza safari ya kazi kama mwimbaji akiwa jijini Lagos, alikua akiimba katika studio za Klink Studios zinazomilikiwa na mtengeneza filamu Kingsley Ogoro. Akiwa hapo aliimarisha kipaji chake na kuendele kufanya kazi za kuingiza viitikio na matangazo katika stesheni mbalimbali za redio na televisheni.

Damasus ni mhitimu kutoka chuo kikuu cha Lagos ambapo alikua mcheza maigizo ya majukwaani. Alitokeza kwa mara ya kwanza katika filamu ya Abused mwaka 1992.[7][8] Filamu iliyompatia umaarufu zaidi ilikua ya pili kuigiza, kwa jina la Breaking Point ya mwaka 1996 iliyoandaliwa na Emem Isong na kuongozwa na Francis Agu, ilimpatia umaarufu mwingi nchini Nigeria. Aliteuliwa katika tuzo za African Movie Academy Award mwaka 2006 katika kipengele cha Muigizaji bora wa kike kutoka katika filamu ya Behind closed doors. Aliteuliwa pia katika tuzo za mwaka 2008,katika kipengele cha mwigizaji bora wa kike kutoka katika filamu ya Widow na mwaka 2009 katika filamu ya State of the Heart. Ameigiza kama mhusika mkuu katika filamu zaidi ya 70.[7][9] na sasa ni mwanzilishi wa kituo cha redio kwa jina la I2radio na muendesha vipindi vya podcast kwa majina ya undiluted with stella damasus na when women praise.

Mwaka Jina Mhusika mkuu
Betrayed by Love Emeka Ike
1999 Face of a Liar Zulu Adigwe, Rita Dominic, Bibiana Ohio
2001 Rumours Segun Arinze, Zulu Adigwe, Kunle Coker, Uche Jombo
2002 Submission Patience Ozokwor, Zack Orji, Clem Ohameze, Jennifer Eliogu
2003 Real Love Ramsey Nouah Jnr, Chioma Chukwuka, Olu Jacobs
2003 Passions Emeka Ike, Richard Mofe Damijo, Genevieve Nnaji, Florence Onuma
2003 My Time 1&2 Bob Manuel Udokwu, Patience Ozokwor, Mary Ann Apollo, Ofia Afuluagu Mbaka
2003 When God says Yes Richard Mofe Damijo, Clem Ohameze, Ngozi Ezeonu, Pete Edochie
2003 Never say goodbye Fabian Adibe, David Ihesie, Ramsey Nouah Jnr
2003 Market seller 1&2 Lilian Bach, Omotola Jalade Ekeinde, Kanayo O Kanayo
2003 The Intruder 1&2 Enebeli Elebuwa, Rita Dominic, Jim Iyke, RMD
2003 Emotional Pain Eucharia Anunuobi, Richard Mofe Damijo, Frank Dallas
2003 Dangerous Desire Fred Amata, Bimbo Akintola, Dayo Adewunmi
2003 Bad Boys Ramsey Nouah Jnr, Clem Ohameze, Amaechi Muonagor
2003 After the Fight Eucharia Anunuobi Ekwu, Kanayo O Kanayo
2004 Queen 1&2 Robert Peters, Richard Mofe Damijo, Nkiru Sylvanus
2004 Missing Angel 1,2&3 Desmond Elliot, Empress Njamah, Nobert Young, Tuvi James
2004 Kings Pride Richard Mofe Damijo, Fred Aresoma, Peter Bruno
2004 Engagement Night 1&2 Richard Mofe Damijo, Darlene Benson-Cobham
2004 Above Love Desmond Elliot, Bukky Wright, Enebeli Elebuwa
2004 Red Hot Liz Benson, Zack Orji, Segun Arinze
2004 Burning Desire 1&2 Richard Mofe Damijo, Enebeli Elebuwa, Ernest Asuzu
2004 Cinderella Desmond Elliot, Grace Amah, Segun Arinze
2004 Dangerous Twins 1, 2 & 3 Ramsey Nouah Jnr, Bimbo Akintola, Lanre Balogun, Sola Sobowale
2005 Wheel of Change Fred Amata, Rita Dominic, Mbong Odungide
2005 The Seed 1&2 Emeka Enyiocha, Chidi Mokeme, Ashley Nwosu
2005 Desperate and Dangerous Chidi Mokeme, Steph-Nora Okereke
2005 Real Love 2&3 Ramsey Nouah Jnr, Caroline Ekanem, Olu Jacobs
2005 Games Women Play 1&2 Genevieve Nnaji, Omotola Jalade Ekeinde, Desmond Elliot, Bob Manuel Udokwu, Zack Orji
2005 The Bridesmaid Richard Mofe Damijo, Kate Henshaw Nuttal, Chioma Chukwuka
2005 Behind Closed Doors 1&2 Desmond Elliot, Richard Mofe Damijo, Patience Ozokwor
2005 Widow Yemi Solade, Peter Bruno
2006 Standing Alone Richard Mofe Damijo, Tony Umez, Jennifer Eliogu
2008 Yankee Girls Omotola Jalade-Ekeinde, Rita Dominic
2008 Yankee Girls 2 Omotola Jalade-Ekeinde, Rita Dominic
2008 Four sisters
2008 Halimat
2016 Affairs of the Heart[10] Pia walihusika Beverly Naya, Divine Shaw, Stephanie Stephen, Glenn Turner, Joel Rogers, Monica Swaida and Cyceru Ash.
2018 Between
  1. Adetu, Bayo. "At 34, Stella Damasus Has No Regrets", P.M. News, 24 April 2012. Retrieved on 1 February 2013. 
  2. Ayakoroma, Barclays Foubiri (2015). Trends in Nollywood: A Study of Selected Genres UPCC book collections on Project MUSE. Kraft Books. ISBN 978-9-78-9182-01-5.
  3. "Nigeria Entertainment Awards 2007". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-10-24. Iliwekwa mnamo 1 Juni 2017.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Biography at OnlineNigeria.com". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2018-10-05. Iliwekwa mnamo 25 Novemba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Clifford, Igbo. "Stella Damasus Biography, Age, Early Life, Family, Education, Career, Net Worth And More". Information Guide Africa. Iliwekwa mnamo 2020-04-26.
  6. "Stella Damasus: Daniel Ademinokan Left His Wife Bcos I Love Him, Our Marriage 'll Last Forever | NaijaGistsBlog Nigeria, Nollywood, Celebrity ,News, Entertainment, Gist, Gossip, Inspiration, Africa". naijagists.com. Iliwekwa mnamo 2016-11-12.
  7. 7.0 7.1 "Quick Fact: Stella Damasus first appeared in ‘Abused’ in 1992", Nigerian Entertainment Today. Retrieved on December 29, 2017. 
  8. "Damasus-Aboderin's first movie". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 18 Septemba 2009. Iliwekwa mnamo 25 Novemba 2009. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help); More than one of |archivedate= na |archive-date= specified (help); More than one of |archiveurl= na |archive-url= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  9. "List of movies by Stella Damasus-Aboderin at the Internet Movie Database". Iliwekwa mnamo 25 Novemba 2009.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  10. "Affairs Of The Heart Watch Stella Damasus and Joseph Benjamin in new movie". Pulse Nigeria. Gbenga Bada. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-03-10. Iliwekwa mnamo 29 Mei 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)