Nenda kwa yaliyomo

Sisini na wenzake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wafiadini walivyochorwa na Paolo Naurizio (1583).

Sisini na wenzake Martiri na Aleksanda (walifariki Sanzeno, karibu na Trento, Italia Kaskazini, 29 Mei 397) walikuwa Wakristo kutoka Kapadokia, leo nchini Uturuki, waliotumwa na askofu mkuu Ambrosi wa Milano kama wamisionari huko Trento kwa ombi la askofu Vijili.

Sisini alikuwa shemasi, Martiri msomaji na Aleksanda bawabu wa kanisa.

Baada ya kujenga kanisa walipokuwa wanamtolea Mungu tenzi za sifa, waliuawa na Wapagani kwa kuchomwa moto[1].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao ni tarehe 29 Mei[2].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  • A. Quacquarelli e I. Rogger (curr.), I martiri della Val di Non e la reazione pagana alla fine del IV secolo (atti del convegno tenuto a Trento il 27-28 marzo 1984), Bologna, EDB, 1985.
  • Réginald Grégoire (cur.), L'Anaunia e i suoi martiri. XVI centenario dei martiri d'Anaunia 397-1997, Trento, Civis, 1997.

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.