Shinto

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Geti ya torii kwenye hekalu ya Kishinto

Shinto au Ushinto ni dini ya kizalendo nchini Japani. Hadi Vita Kuu ya Pili ya Dunia ilikuwa dini rasmi ya serikali na ya Kaisari wa Japan.

Imani ya Shinto ni katika miungu au mapepo wengi wanaoitwa "kami". Wengine wao ni kama miungu wengine ni roho za miti, mito au milima tena wengine ni roho za wazimu. Kati ya kami muhimu zaidi ni amaterasu (jua), dunia, mbingu.

Kuna makuhani wanaotunza hekalu ambako sadaka hutolewa kwa kami hizi. Wajapani wengi hushiriki katika ibada za kami wakikumbuka marehemu na mababu hata wakifuata dini nyingine kama Ubuddha au Ukristo.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Icon-religion.png Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Shinto kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.