Seneriko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu ya Mt. Seneriko katika mavazi ya kikardinali.

Seneriko (pia: Cerenico, Cinereo, Serenidus, Cénéré, Sénéré, Sérène, Sérenède; Spoleto, Italia, 600 hivi - Le Mans, Ufaransa, 7 Mei 669 au 680) alikuwa mmonaki shemasi ambaye, baada ya kuhiji kwenye makaburi ya Martino wa Tours na Juliani wa Le Mans, alishika maisha magumu upwekeni; inasemekana akaanzisha monasteri yenye watawa 140[1].

Inasemekana pia kwamva alipokuwa kijana alifanywa kardinali na Papa Martin I[2] .

Anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 7 Mei[3].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. http://www.santiebeati.it/dettaglio/52110
  2. Saint Céréné (fr).
  3. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.