Say Somethin'

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
“Say Somethin'”
“Say Somethin'” cover
Single ya Mariah Carey featuring Snoop Dogg
Imetolewa Aprili 3, 2006 (2006-04-03)
(See release history)
Muundo Digital download, CD single
Aina Pop, R&B, hip hop
Urefu 3:44
Studio Island
Mtunzi Mariah Carey, Chad Hugo, Pharrell Williams, Snoop Dogg
Mtayarishaji The Neptunes


"Say Somethin'"
(2006)

"Fly Like a Bird"
(2006)
Mwenendo wa za Snoop Dogg
"Gangsta Zone"
(2005)
"Say Somethin'"
(2006)
"Buttons"
(2006)

"Say Somethin'" ni wimbo ulioandikwa na Mariah Carey akishirikiana na Snoop Dogg, Chad Hugo, wakishirikiana na Pharrell Williams kwa ajili ya albamu ya Carey ya kumi iliyoitwa The Emancipation of Mimi iliyotoka mwaka 2005. Mwimbaji Snoop Dogg anatokezea katika wimbo huu kama mwanamuziki wa kushirikishwa na anaimba shairi moja. Wimbo huu unajumuisha waimbaji mbalimbali na ulifanikiwa kutoka rasmi mwaka 2006, kama single ya sita kutoka katika albamu hii. Wimbo huu ulifanikiwa kufika katika nyimbo arobaini bora nchini Australia na Uingereza, lakini nchini Marekani wimbo huu haukufanikiwa kuingia hata katika chati ya Billbord Hot 100.

Utunzi na Maudhui[hariri | hariri chanzo]

Wimbo wa "Say Somethin'" na "To the Floor" ambao pia umeandikwa na The Neptunes, na wimbo mwingine kutoka katika albamu ya The Emancipation of Mimi, ndio nyimbo za kwanza tangu kutoka kwa albamu ya Mariah Carey ambazo yeye mwenyewe hajashiriki katika kuziandaa. Kundi la The Neptunes limejiwekea sheria kali kuwa, hawatarusu kuhusisha wanamuziki wengine kushiriki katika kuandaa nyimbo zao isipokuwa Beyonce Knowles, B'Day na Madonna. Ijapokuwa Carey aliyamani kufanya kazi na kundi hili lakini haikuwezekana kutayarisha wimbo hata mmoja.

Mashairi ya wimbo huu, yanaelezea watu wawili wanaotambulishwa katika ukumbi wa usiku. Kila mmoja anajaribu kuonyesha hisia za kimapenzi lakini kila mmoja anasubiri mwenziwe aanze kumwambia mwenzake. Hatimaye mwanamke anashindwa kuvumilia na kuanza kuonyesha hisia zake kwa mwanaume.

Historia[hariri | hariri chanzo]

"Say Somethin'" ulikuwa ni wimbo wa kwanza kutoka katika albamu ya The Emancipation kuingia katika wavuti ilipofanya hivyo mwezi Novemba mwaka 2004. Wavuti mbalimbali za nyimbo na maduka mengine ya nyimbo, MTV chati ya Billboard ziliripoti kuwa wimbo huo uliwa na mafanikio katika redio mbalimbali. .[1] Japokuwa Carey hapo awali alitaka wimbo wa Say Something utoke kama singe ya kwanza, lakini Carey aliendelea kupigania kutoka kwa wimbo wa Shake It Off utoke kama single ya kwanza.Kampuni yake ya kurekodia hatimaye iliamua kuacha wimbo wa Shake It Off utoke kama single ya kwanza badala ya wimbo wa Say Something

Wimbo huu baadae ulitoka kama single ya tatu nje ya Marekani na nchini Uingereza. Pia kulikuwa na tetesi kuwa wimbo huu ndio ulikuwa single ya mwisho nchini Marekani lakini Studio za Carey bado zilitaka kutoa single nyingine katika albamu ya The Emancipation of Mimi, huku single ya tatu ikiwa katika single mpya kutoka "Don't Forget About Us".

Mapokezi[hariri | hariri chanzo]

Wimbo wa "Say Somethin'" ulipata mapokeo tofauti tofauti kutoka kwa wanamuziki mbalimbali, kama vile mwimbaji Bill Lamb wa kundi la About.com alisema Hatimaye wimbo huu umetoka sasa, na ni tukio la aina yake, kwa kuwa na sauti za kuvutia kama vile ya Mariah Carey na Snoop Dogg, hakuna la zaidi tunalosubiaria ."[2] Nchini Uingereza wimbo huu, haukufanya vizuri sana kama zilivyokuwa kwa single zilizopita, ilifanikiwa kufika katika nafasi ya 27. na kukaa katika chati hii kwa juma moja.

Picha:SaySomethin'ScreenShot.jpg
Mariah Carey wakati wa utengenezaji wa wimbo huu akiwa kitandani

Mundo na Orodha ya nyimbo[hariri | hariri chanzo]

European CD single

  1. "Say Somethin'" (Album Version)
  2. "Say Somethin'" (Morales Radio Edit)

Australian/European CD maxi-single

  1. "Say Somethin'" (Album Version)
  2. "Say Somethin'" (Stereo Anthem Mix)
  3. "Say Somethin'" (Stereo Dub)
  4. "Say Somethin'" (Video)

Chati[hariri | hariri chanzo]

Chati (2006) Ilipata
nafasi
Australian Singles Chart[3] 26
Belgium Ultratip Chart (Flanders)[4] 3
Belgium Ultratip Chart (Wallonia)[4] 10
European Singles Chart[5] 60
German Singles Chart[6] 63
Irish Singles Chart[7] 23
Swiss Singles Chart[8] 55
UK Singles Chart[9] 27
U.S. Billboard Hot 100[10] 79
U.S. Billboard Hot Dance Club Play[10] 1

Historia ya kutoka[hariri | hariri chanzo]

Nchi Tarehe ya kutoka
United States Aprili 3, 2006 (2006-04-03)
United Kingdom Juni 5, 2006 (2006-06-05)

Marejeo[hariri | hariri chanzo]