Salamu Maria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kupasha Habari, kadiri ya Fra Angelico.

Salamu Maria (kwa Kilatini Ave Maria) kwa asili ni sala ya Wakatoliki wa Kanisa la Kilatini ambayo inamsifu Bikira Maria na kumuomba sala zake hadi saa ya kufa.

Sala hiyo imeenea hata kwa Wakristo wengine, hasa Waanglikana, lakini kwa namna tofauti inatumiwa pia katika Ukristo wa Mashariki.

Hii ni kwa sababu sehemu kubwa ya sala hiyo inatokana na Injili (Lk 1:28,42) moja kwa moja:

  • Χαῖρε, κεχαριτωμένη, ὁ Κύριος μετὰ σοῦ / Chaire, kecharitōmenē, o Kyrios meta sou / Salamu uliyejaa neema, Bwana yu nawe (maneno ya Malaika Gabrieli)
  • Εὐλογημένη σὺ ἐν γυναιξὶν καὶ εὐλογημένος ὁ καρπὸς τῆς κοιλίας σου / eulogēmenē su en gynaixin kai eulogēmenos o karpos tēs koilias sou / Umebarikiwa wewe kati ya wanawake na umebarikiwa mzao wa tumbo lako (maneno ya Elizabeti)

Katikati ya karne ya 13 sala ilikuwa inaundwa na maneno hayo tu pamoja na kuingiza jina la Maria, inavyoonekana katika ufafanuzi wa Thoma wa Akwino.[1]

Mwishoni mwa karne ya 15 yaliongezwa maneno ya kumuomba Maria sala zake.[2]

Hatimaye sala kwa Kilatini imekuwa hivi:

Áve María, grátia pléna,
Dóminus técum.
Benedícta tu in muliéribus,
et benedíctus frúctus véntris túi, Iésus.[3]
Sáncta María, Máter Déi,
óra pro nóbis peccatóribus,
nunc et in hóra mórtis nóstrae. Ámen.

Tafsiri ya Kiswahili ni:

Salamu María, umejaa neema,
Bwana yu nawe.
Umebarikiwa kuliko wanawake wote,
na Yesu, mzao wa tumbo lako, amebarikiwa.
Maria Mtakatifu, Mama wa Mungu,
utuombee sisi wakosefu,
sasa na saa ya kufa kwetu. Amina.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Saint Thomas Aquinas on the Hail Mary", Catholic Dossier, May-June 1996, Ignatius Press, Snohomish, Washington. Jalada kutoka ya awali juu ya 2015-09-24. Iliwekwa mnamo 2015-11-07.
  2. British Library - Rare Books Department, shelfmark: IA 27542
  3. With Pope John XXIII's edition of the Roman Missal, the use of the letter J in printing Latin was dropped even in liturgical books, which had preserved that usage long after it ceased in the printing of ordinary Latin texts, including documents of the Holy See.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Salamu Maria kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.