Rugu
Kata ya Rugu | |
Nchi | Tanzania |
---|---|
Mkoa | Kagera |
Wilaya | Karagwe |
Idadi ya wakazi | |
- Wakazi kwa ujumla | 6,990 |
Rugu ni jina la kata ya Wilaya ya Karagwe katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye postikodi namba 35407 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 14,160 waishio humo.[2]
Kata ya Rugu inapatikana upande wa Kusini-Mashariki mwa Wilaya ya Karagwe. Hasa inapakana na Ziwa Burigi pamoja na Hifadhi ya Wanyama Burigi kwa upande wa Kusini. Mashariki kuna Wilaya ya Muleba, Magharibi ni kata jirani ya Nyakasimbi na Kaskazini ni Kata za Nyaishozi (Kaskazini Magharibi) na Ihembe (Kaskazini Mashariki).
Kata ya Rugu ina idadi ya jumla ya vijiji vitano. Vijiji hivyo ni Kasheshe, Misha, Rugu, Ruhita, Misha.
Elimu[hariri | hariri chanzo]
Kata ya Rugu ni moja kati ya kata zenye wazazi wanaopenda kuchangia mafanikio ya Ukuaji wa Elimu ikiwa mwaka 2010 wazazi walichangia kununua vifaa vya sayansi na hivyo kuifanya Shule ya Sekondari Rugu kuwa na maabara mapema sana.
Kata ya Rugu ina shule moja ya sekondari iitwayo Rugu Shule ya Sekondari, na shule nne za msingi ambazo ni Shule ya Msingi: Kasheshe, Misha, Ruhita na Rugu.
Utamaduni[hariri | hariri chanzo]
Lugha inayotumiwa na raia wa kata ya Rugu hasa ni Kinyambo (kwa kilugha Runyambo).
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
- ↑ Nakala iliyohifadhiwa. Jalada kutoka ya awali juu ya 2018-08-05. Iliwekwa mnamo 2018-02-01.
- ↑ Sensa ya 2012, Kagera - Karagwe-District-Council
![]() |
Kata za Wilaya ya Karagwe - Mkoa wa Kagera - Tanzania | ![]() |
---|---|---|
Bugene | Bweranyange | Chanika | Chonyonyo | Igurwa | Ihanda | Ihembe | Kanoni | Kayanga | Kibondo | Kihanga | Kiruruma | Kituntu | Ndama | Nyabiyonza | Nyaishozi | Nyakabanga | Nyakahanga | Nyakakika | Nyakasimbi | Rugera | Rugu |
![]() |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Rugu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |