Nenda kwa yaliyomo

Rostam Abdulrasul Aziz

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Rostam Aziz)

'

Rostam Abdulrasul Aziz
Amezaliwa21 Agosti 1964
Kazi yakemfanyabiashara


Rostam Abdulrasul Aziz (amezaliwa 21 Agosti 1964) ni mfanyabiashara / mjasiriamali na mwanasiasa kutoka Tanzania. Aliripotiwa mnamo 2013 kuwa bilionea wa kwanza wa dolar za Marekani nchini Tanzania, akimiliki mali ya jumla ya thamani ya dolar bilioni 1. [1]

Alikuwa mbunge wa jimbo la Igunga katika Mkoa wa Tabora kuanzia mwaka 1994 hadi alipojiuzulu mwaka 2011. [2] Alikuwa mtunza hazina wa kitaifa wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kutoka 2005 hadi 2007 na mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM kutoka 2006 hadi 2011.

Katika jimbo lake la uchaguzi alianzisha mradi wa bima ya afya ya jamii iliyokuwa wa kwanza katika Afrika Mashariki ambako kila kaya katika jimbo lake ilipatiwa bima ya afya kutoka Mfuko wa Afya ya Jamii. Alipanua pia mfumo wa maji hadi kila mkazi katika jimbo lake aliweza kutumia maji safi. Jimbo la Igunga liliendelea kuwa wilaya ya kwanza ya Tanzania yenye kituo cha afya katika kila kijiji na umeme katika kila kata.

Kulingana na gazeti la Forbes [3] Rostam Aziz mnamo mwaka 2016 alimiliki karibu 18% ya Vodacom Tanzania ambayo ni kampuni kubwa ya simu za rununu nchini, yenye wanachama 15,000,000. [4] Rostam aliwahi kushika asilimia 35 za hisa za Vodacom kupitia kampuni yake ya Cavalry Holdings, lakini kwenye Mei 2014 aliuza asilimia 17.2 za hisa za Vodacom Tanzania kwa Vodacom Group ya Afrika Kusini kwa bei iliyokadiriwa kuwa $ milioni 250. [5]

Anamiliki pia kampuni ya Caspian Mining inayochimba migodi na kutekeleza miradi ya ujenzi[6], pamoja na kuwa na nyumba huko Dubai na Oman.

Aziz alianza biashara katika kampuni ya familia yake akaendelea kujenga himaya yake menyewe.

Rostam alizaliwa katika familia ya Wabaluchi Watanzania waliofika kutoka Uajemi na kukaa nchini tangu vizazi vitano. [7] Wamekaa Tanganyika baada ya kufika awali huko Zanzibar mnamo 1850. Mwanzoni familia ilianza kama wakulima wa katani, mchele na miwa.

  1. "50 RICHEST PEOPLE IN AFRICA #26Rostam Azizi". Forbes. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-05-10. Iliwekwa mnamo 21 Julai 2015. Rostam Azizi, Tanzania's first billionaire.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. Guardian, Reporter (13 Julai 2011). "Rostam Resigns As MP, NEC Member". IPP Media (Dar es Salaam). Iliwekwa mnamo 6 Novemba 2014.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  3. "Rostam Azizi". Forbes. Iliwekwa mnamo 31 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  4. "Vodacom Group Wraps Up Stake Acquisition From Rostam Aziz". WealthX. 6 Mei 2014. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-03-25. Iliwekwa mnamo 17 Julai 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  5. Nsehe, Mfonobong. "Tanzania's Richest Man Concludes Sale Of Vodacom Stake". Forbes. Iliwekwa mnamo 31 Mei 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
  6. "Nakala iliyohifadhiwa". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-06-21. Iliwekwa mnamo 2020-06-20.
  7. David Lawrence (Oktoba 2009). Tanzania: The Land, Its People and Contemporary Life. Intercontinental Books. ku. 26–. ISBN 978-9987-9308-3-8.{{cite book}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Rostam Abdulrasul Aziz kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.