Rosaline Meurer
Rosaline Ufuoma Meurer (kuzaliwa 15 Februari 1992), ni mtayarishaji na mcheza filamu wa Nigeria, mzaliwa wa Gambia.[1][2] Anajulikana sana kwa uhusika wake katika filamu ya Oasis ya waka 2014 pamoja na uhusika wake kama Kemi Alesinloye katika filamu iliyoandaliwa na Ayo Makun kwa jina la Merry Men: The Real Yoruba Demons mwaka 2018.[3][4]
Maisha ya Mwanzo na Elimu
[hariri | hariri chanzo]Meurer alikulia nchini Gambia ambapo alipata elimu yake ya msingi. Ana astashahada ya usimamizi wa biashara na pia alisomea upigaji picha.[5]
Kazi
[hariri | hariri chanzo]Katika umri wake mdogo, Meurer alipenda sana Ndege (uanahewa) na vyombo vya kupaa, alitamani aje kua mhudumu wa ndege au hata rubani. Alianza kazi kama mwanamitindo akiwa nchini Gambia, kabla ya kuhamia Nigeria mwaka 2009. Kipaji chake kilionekana na muigizaji na mwanasiasa Desmond Elliot akiwa Gambia mwaka 2009, ambaye alimshauri aanze kujaribu kuigiza nchini Nigeria.[6] Alihamia Lagos, Nigeria na kuanza kazi ya kucheza filamu, alianza katika filamu ya Emem Isong kwa jina la Spellbound mwaka 2009, mwaka 2011 katika filamu ya In the Cupboard (film)|In the Cupboard.[7][8]
Mwaka 2012, alihusika katika filamu ya Weekend Getaway.[9] Baada ya uhusika wake katika filamu hiyo ya mwaka 2012, aliacha kazi ya uigizaji kwa muda na kurudi masomoni nchini Gambia, baadaye alirudi tena nchini Nigeria na kuendelea na kazi ya uigizaji. Aliporudi mwaka 2014, alikua miongoni mwa wahusika katika filamu ya Oasis, akiwa mhusika kwa jina la Kaylah.[10][11] Mwaka uliofuatia, alicheza kama Nneka katika filamu ya Damaged Petal, alishiriki pia katika filamu ya Red Card na Open Marriage.[12]
Mwaka 2017, alikua mhusika mkuu katika filamu ya Our Dirty Little Secret.[13] Mwaka huohuo, alikua mhusika kwa jina la Monica katika maonyesho ya televisheni kwa jina la Philip and Polycarp alishiriki pia katika filamu ya The Incredible Father, Pebbles of Love na Our Dirty Little Secret.[14] Baadaye aliachia filmu yake ya kwanza kwa jina la The Therapist's Therapy.[15] Mwaka 2018, alihusika kama Valerie katika filamu ya Eniola Badmus kwa jina la Karma na pia aliigiza kama Kemi Alesinloye katika filamu ya Ayo Makun kwa jina la Merry Men: The Real Yoruba Demons.[16][17][11]
Uhisani
[hariri | hariri chanzo]Mnamo Mei 25 2017, Meurer aliongoza katika kukarabati mradi wa maji wa soko kuu ya Udu, Udu, Nigeria|Udu, jimbo la Delta.[18][19] Kama balozi wa makanisa makubwa ya usimamizi wa wanawake na Watoto, alitoa msaada katika kliniki ya wanawake wajawazito na wazazi iliyopo Warri, jimbo la Delta.[20][21]
Ubia Mwingine
[hariri | hariri chanzo]Meurer ni balozi wa Multisheen Ebony.[22] Mwaka 2015, aliteuliwa kua balozi wa “Big Church Foundation on Women and Child”.[23][24] Alitokeza katika ukurasa wa mbele wa jarida la mwezi Aprili 2017 House Of Maliq Magazine.[25] Mnamo Aprili 2019, alitia Saini ya idhini na DoctorCare247.[26] Miezi minne baadae, alisaini idhini nyingine na Glo.[22][27]
Maisha binafsi
[hariri | hariri chanzo]Meurer alizaliwa Gambia, baba yake ni mholanzi na mama yake anatokea jimbo la Delta nchini Nigeria. Ni mzaliwa wa kwanza katika familia yenye Watoto watatu.[28][11]
Sanaa
[hariri | hariri chanzo]Filamu
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
2009 | Spellbound | ||
2011 | In the Cupboard | ||
2012 | Weekend Getaway | ||
2015 | Damaged Petal | Nneka | |
2015 | Red Card | Kachi | |
2015 | Open Marriage | Becky | |
2016 | My Sister And I | ||
2017 | Pebbles of Love | Vanessa | |
2017 | Our Dirty Little Secret | Anita | |
2017 | The Incredible Father | Susan | |
2018 | Merry Men: The Real Yoruba Demons | Kemi Alesinloye | |
2018 | Karma | Valerie | |
2019 | Accidental Affair | Jenny | |
2020 | Circle of Sinners | Betty | |
TBA | Table of Men |
Televisheni
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Jina | Uhusika | Maelezo |
---|---|---|---|
2014 | Oasis | Kaylah | Mhusika mkuu |
2017 | Philip and Polycarp | Monica | Mhusika mkuu |
Tuzo na Teuzi
[hariri | hariri chanzo]Mwaka | Tuzo | Kipengele | Matokeo | Rej |
---|---|---|---|---|
2017 | City People Movie Awards | Muigizaji bora wa kike chipukizi | mshiriki | [29] |
La Mode Green | Tuzo maalumu ya utambuzi | Mshindi | [30] | |
2016 | Nigeria Goodwill Ambassador Awards | Muigizaji bora ajae | Mshindi | [31] |
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ "Tonto Dikeh's ex, Churchill declares love for Rosy Meurer". P.M. News. 15 Februari 2020. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ogbeche, Danielle. "Lady accused of having sex with Tonto Dikeh’s husband blasts critics", Daily Post Nigeria, 19 January 2017. Retrieved on 15 May 2020.
- ↑ "Nigeria: Top 10 Young Actresses to Look Out for in 2018", AllAfrica.com, 4 March 2018. Retrieved on 15 May 2020. Archived from the original on 5 March 2018.
- ↑ "'Merry Men' Back On Another Mission". This Day Newspaper. 14 Desemba 2019. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Rosaline Meurer bags 'indigenous Woman award'". Vanguard Newspaper. 12 Julai 2019. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "I got more jobs, money after Tonto Dikeh's marriage crisis allegations – Rosaline Meurer". The Punch Newspaper. 8 Aprili 2018. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Spellbound". Modern Ghana. 23 Machi 2011. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Skeletons in their closet - ‘In the cupboard’ film review", Daily Post Nigeria, 14 September 2012. Retrieved on 15 May 2020.
- ↑ Okiche, Wilfred. "Film review: ‘Weekend Getaway’ gathers all the stars, but has no idea what to do with them", YNaija, 5 May 2013. Retrieved on 15 May 2020.
- ↑ "'At 26 I have achieved what some of you can never achieve'- Rosy Meurer tells age doubters". Lailas News. 7 Julai 2018. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-04-13. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 11.0 11.1 11.2 Onuorah, Vivian (19 Februari 2017). ""I Didn't Break TONTO DIKEH's Marriage, Ask Her"--ROSALINE MEURER". City People Magazine. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Boulor, Ahmed. "Lady accused of dating Tonto Dikeh’s husband cries out (Video)", Ripples Nigeria, 19 January 2017. Retrieved on 15 May 2020.
- ↑ "Society doesn't allow Nigerian women to be romantic – Daniel Lloyd". Vanguard Newspaper. 24 Septemba 2017. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "#BNMovieFeature: WATCH IK Ogbonna, Daniel Lloyd, Rosaline Meurer, Stan Nze in "Pebbles of Love"", BellaNaija, 11 August 2019. Retrieved on 15 May 2020.
- ↑ Nathaniel, Nathan (16 Septemba 2017). "Actress Rosaline Meurer Joins League Of Movie Producers". The Nigerian Voice. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ McCahill, Mike. "Merry Men: The Real Yoruba Demons review – cheerful comedy, lost in translation, Film", The Guardian, 7 December 2018. Retrieved on 15 May 2020.
- ↑ Efe, Obiomah. "Merry Men:The Real Yoruba Demons is amoral", flickchat, 30 September 2018. Retrieved on 15 May 2020.
- ↑ "Actress Rosaline Meurer Commissions Water Project". This Day Newspaper. 16 Julai 2017. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Nathaniel, Nathan (10 Julai 2017). "Actress, Rosaline Meurer Gives Life To Udu Community As She Commissions New Water Project". The Nigerian Voice. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Onuoha, Chris (28 Mei 2017). "Nollywood actress Rosaline Meurer donates cash to pregnant women". Vanguard Newspaper. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Adebayo, Tireni (28 Mei 2017). "Nollywood actress Rosaline Meurer donates cash to pregnant women". Kemi Filani News. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ 22.0 22.1 "Actress Rosaline Meurer Becomes GLO Ambassador". The Herald Newspaper. 22 Agosti 2019. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Bivan, Nathaniel. "Nigeria: Praiz Becomes Ambassador for Charity", AllAfrica.com, 25 February 2017. Retrieved on 15 May 2020. Archived from the original on 26 February 2017.
- ↑ Olushola, Ricketts (28 Aprili 2019). "Why I'm still close to Tonto Dikeh's ex-husband –Rosaline Meurer". The Punch Newspaper. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Olukomaiya, Funmilola (18 Aprili 2017). "Jumoke Orisaguna, Rosaline Meurer Cover House Of Maliq Magazine". P.M. News. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Olushola, Ricketts (8 Mei 2019). "DoctorCare247 to tackle health challenges in Nigeria". The Punch Newspaper. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Ngere, Ify Davies (20 Agosti 2019). "Tonto Dikeh's Ex-Husband, Showers Accolades On Actress, Rosaline Meurer As She Bags Endoresment Deal". Within Nigeria. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Interesting! 10 Top Facts You Must Know About Controversial Actress Rosaline Meurer", Naijaloaded, 7 February 2017. Retrieved on 15 May 2020.
- ↑ Omaku, Josephine (12 Septemba 2017). "City People Movie Awards: and the Nominees are…". Ghafla!. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-24. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: More than one of|accessdate=
na|access-date=
specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ Nathaniel, Nathan (10 Julai 2017). "Rosaline Meurer Bags Special Award for ambassadorial support for mother and child". The Nigerian Voice. Iliwekwa mnamo 15 Mei 2020.
{{cite web}}
: CS1 maint: date auto-translated (link) - ↑ "Nigeria: Kudos!!! Pretty Nollywood Star, Roseline Meurer Nominated for Nigeria Goodwill Ambassador Awards 2016", AllAfrica.com, 16 November 2016. Retrieved on 15 May 2020. Archived from the original on 18 November 2016.