Tuwanyika
Mandhari
(Elekezwa kutoka Rhamphiophis)
Tuwanyika | ||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Tuwanyika kahawianyekundu (Rhamphiophis rostratus)
| ||||||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||||||
| ||||||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||||||
Spishi 3:
|
Tuwanyika, domotai au nondo ni spishi za nyoka wa jenasi Rhamphiophis katika familia Lamprophiidae. Nyoka hawa ni warefu kiasi: kwa kipeo m 1.5-2.5 kulingana na spishi. Rangi yao ni kijivu, kahawia, pinki, machungwa au nyeupe. Kichwa ni kifupi, pua ndefu na macho makubwa.
Tuwanyika huingia mashimo ndani ya ardhi mara nyingi ili kupumzika au kutafuta mawindo yao: wagugunaji, mijusi, vyura na hata nyoka wengine. Wanaweza kuwinda katika vichaka pia.
Chonge zao ni meno ya nyuma kabisa lakini wanaweza kuingiza sumu waking'ata mtu. Hata hivyo sumu yao haina hatari sana kwa watu; inaweza kusababisha maumivu ya kichwa. Wakikaribishwa hutoroka au wasipoweza wanapanua shingo kwa ukaya na kuinua sehemu mbele ya mwili kama fira.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Rhamphiophis oxyrhynchus Tuwanyika Magharibi (Western beaked snake)
- Rhamphiophis rostratus Tuwanyika Kahawianyekundu (Rufous beaked snake)
- Rhamphiophis rubropunctatus Tuwanyika Kichwa-machungwa (Red beaked snake)
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Tuwanyika kichwa-machungwa
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Spawls, S., Howell, K., Drewes, R. & Ashe, J. (2002) A field guide to the Reptiles of East Africa. Academic Press, San Diego, CA, USA.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]Makala hii kuhusu mnyama fulani bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Tuwanyika kama uainishaji wake wa kibiolojia, maisha au uenezi wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |