Nenda kwa yaliyomo

Rais wa Nigeria

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rais wa Nigeria Bola Tinubu

Rais wa Nigeria ni mkuu wa dola wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria na kiongozi wa serikali. Vyeo vyake ni "Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Nigeria" na Amiri Jeshi Mkuu wa jeshi la Nigeria. Rais wa sasa ni Bola Tinubu.

Masharti[hariri | hariri chanzo]

Kila mtu anaweza kuchaguliwa kuwa rais wa Nigeria kama

 • yeye ni raia wa Nigeria
 • umri wake ni miaka 40 au zaidi
 • ni mwanachama wa chama cha kisiasa nchini na kukubaliwa na chama hiki

Kufuatana na katiba anaweza kuhudumia awamu mbili za miaka minne akichaguliwa tena baada ya awamu ya kwanza.

Madaraka ya rais wa Nigeria[hariri | hariri chanzo]

Kufuatana na katiba rais huwa na madaraka yafuatayo:

 • kukubali na kutia sahihi sheria zilizopitishwa bungeni
 • kurudisha sheria bungeni akiwa na mashaka kama sheria inalingana na katiba
 • kupeleka sheria mbele ya mahakama kuu itakayoamua kama inalingana na katiba
 • kuitisha bunge kwa makao maalumu kwa shughuli za pekee
 • kusimamika maafisa kufuatana na katiba au sheria
 • kusimamika kamati za utafiti
 • kuitisha kura ya wananchi kulingana na sheria
 • kupokea na kutambua mabalozi wa nchi za nje
 • kusimamika mabalozi
 • kusamehe wakosaji waliohukumiwa na mahakama

Orodha ya wakuu wa dola na maraisi wa Nigeria[hariri | hariri chanzo]

Katika orodha ifuatayo kuna majina ya watu waliokuwa wakuu wa dola nchini Nigeria tangu uhuru katika mwaka 1960:

Jina Tarehe za uraisi Alikotoka
Mwanzo Mwisho Namna ya kumaliza kipindi
Abubakar Tafawa Balewa (Waziri Mkuu) 1 Oktoba 1960 15 Januari 1966 Alipinduliwa na jeshi Northern People’s Congress
Nnamdi Azikiwe 1 Oktoba 1963 16 Januari 1966 National Council of Nigeria and the Cameroons
Johnson Aguiyi-Ironsi 16 Januari 1966 29 Julai 1966 Alipinduliwa na jeshi jeshini
Yakubu Gowon 1 Agosti 1966 26 Julai 1975 Alipinduliwa na jeshi Jeshini
Murtala Mohammed 29 Julai 1975 13 Februari 1976 Kifo baada ya kujeruhiwa na waasi wa kijeshi Jeshini
Olusegun Obasanjo 13 Februari 1976 1 Oktoba 1979 Alishindwa katika uchaguzi Jeshini
Shehu Shagari 1 Oktoba 1979 31 Desemba 1983 Alipinduliwa na jeshi National Party of Nigeria
Muhammadu Buhari 31 Desemba 1983 27 Agosti 1985 Alipinduliwa na jeshi Jeshini
Ibrahim Babangida 27 Agosti 1985 26 Agosti 1993 alijiuzulu Jeshini
Ernest Shonekan 26 Agosti 1993 17 Novemba 1993 alijiuzulu (bila chama)
Sani Abacha 17 Novemba 1993 8 Juni 1998 Kifo Jeshini
Abdulsalami Abubakar 8 Juni 1998 29 Mei 1999 Alishindwa katika uchaguzi Jeshini
Olusegun Obasanjo 29 Mei 1999 29 Mei 2007 Alishindwa katika uchaguzi People's Democratic Party
Umaru Yar'Adua 29 Mei 2007 5 Mei 2010 Kifo People's Democratic Party
Goodluck Jonathan 5 Mei 2010 29 Mei 2015 People's Democratic Party
Muhammadu Buhari 29 Mei 2015 29 Mei 2023 All Progressives Congress
Bola Tinubu 29 Mei 2023 All Progressives Congress

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]