Nenda kwa yaliyomo

Goodluck Jonathan

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Goodluck Ebele Azikiwe Jonathan


Aliingia ofisini 
6 Mei 2010
Rais mtendaji: 9 Februari 2010 – 6 Mei 2010
Makamu wa Rais Namadi Sambo
mtangulizi Umaru Yar'Adua

Makamu wa Rais wa Nigeria
Muda wa Utawala
29 Mei 2007 – 6 Mei 2010
Rais Umaru Yar'Adua
mtangulizi Atiku Abubakar
aliyemfuata Namadi Sambo

Gavana wa jimbo la Bayelsa
Muda wa Utawala
9 Desemba 2005 – 28 Mei 2007
mtangulizi Diepreye Alamieyeseigha
aliyemfuata Timipre Sylva

tarehe ya kuzaliwa 20 Novemba 1957
Ogbia, Nigeria
chama People's Democratic Party
ndoa Patience Faka Jonathan
mhitimu wa Chuo Kikuu cha Port Harcourt
Fani yake Zoolojia
dini Ukristo

Goodluck Ebele Azikiwe Jonathan (alizaliwa 20 Novemba 1957)[1] alikuwa rais wa Nigeria tangu Januari 2010. Awali hakuchaguliwa lakini alikabidhiwa madaraka akiwa makamu wa rais mgonjwa Umaru Yar'Adua aliyemtangulia na baada ya kifo chake aliapishwa kama rais. Katika uchaguzi wa kitaifa wa Aprili 2011 alirudishwa madarakani.

Elimu na maisha ya awali

[hariri | hariri chanzo]

Jonathan alizaliwa katika familia ya Wakristo wa kabila ya Ijaw kwenye delta ya mto Niger.[2] Alisoma shule za msingi Otuoke na Oloibiri na tangu 1971 shule ya sekondari ya Mater Dei mjini Imiringi. 1975 hadi 1977 alifanya kazi ya idara ya ushuru na kodi. 1977 akajiandikisha kama mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Port Harcourt katika idara ya zoolojia. Baada ya kumaliza kwa digrii ya bachela alifanya kazi ya ualimu wa shule mjini Iresi. Aliendelea kusoma Chuo Kikuu hadi kupata digrii za MSc na daktari ya falsafa katika zoolojia. 1993 alikuwa makamu wa mkurugenzi wa kamati ya maendeleo ya maeneo ya kutoa mafuta Nigeria akiwajibika kwa mambo ya kuhifadhi mazingira. 1998 aliingia katika siasa.[3]

Jonathan amemwoa Patience Faka Jonathan akiwa na watoto 2 [4]

Maisha ya kisiasa

[hariri | hariri chanzo]

Gavana wa jimbo la Bayelsa

[hariri | hariri chanzo]

Jonathan alijiunga na chama cha People's Democratic Party (PDP) mwaka 1998.[2] 1999 aliteuliwa kuwa makamu wa gavana. Gavana Diepreye Alamieyeseigha aliondolewa madarakani mwaka 2005 kutokana na mashtaka ya rushwa Jonathan alimfuata akawa gavana wa Bayelsa.

Mwaka 2006 mke wa Jonathan alishtakiwa na Halmashauri ya kupambana na rushwa kwa makosa ya kuficha pesa zisizo halali. [5]

Makamu wa rais

[hariri | hariri chanzo]

Mwezi wa Desemba 2006 mgombea wa urais Umaru Yar'Adua alimchagua Jonathan kama makamu wake kabla ya uchaguzi wa kitaifa wa 2007. [6] Kabla ya kura Jonathan alishambuliwa na wanamgambo tarehe 20 Aprili 2007 waliojaribu kumwua bila kufanikiwa. [7]

Baada ya ushindi wa Yar'Adua Jonathan alikuwa makamu wa rais kuanzia tarehe 29 Mei 2007.

Raisi Yar'Adua aligonjeka 2009 akaondoka nchini kwenda Saudia kwa matibabu. Baada ya rais Yar'dua kukaa miezi mfululizo katika hospitali nchini Saudia mahakama kuu ilimpa madaraka ya rais. Yar'Adua alipoaga dunia tarehe 5 Mei 2010 Jonathan aliapishwa siku iliyofuata kuwa rais wa 14 wa Nigeria.

Alimteua aliyewahi kuwa gavana wa jimbo la Kaduna kuwa makamu wake. [8][9]

Jonatahan aligombea urais katika uchaguzi wa 16 Aprili 2011 aliposhinda katika awamu ya kwanza kwa kupata kura 22,495,187 na angalau robo ya kura zote katika theluthi mbili za majimbo ya Nigeria. Mpinzani wake mkuu Buhari wa CPC alipewa kura 12,214,853 pekee. Watazamaji wa kimataifa walitangaza uchaguzi kuwa huru na kweli.[10]

  1. Lawson Heyford, "Jonathan: A Colossus at 49" Ilihifadhiwa 15 Januari 2009 kwenye Wayback Machine., The Source (Lagos), 11 Desemba 2006
  2. 2.0 2.1 http://english.aljazeera.net/news/africa/2010/02/20102247327794647.html
  3. "Profile: Goodluck Jonathan", BBC News, 6 Mei 2010. Retrieved on 6 Mei 2010. 
  4. "Money Laundering: I'm Not Involved, Says Bayelsa Governor", Thisday, via EFCCNigeria.org, Leaders & Company, 2006-09-12. Retrieved on 2007-09-22. Archived from the original on 2006-10-07. 
  5. By Gilbert da Costa / Abuja Saturday, Feb. 13, 2010. "Is Goodluck Jonathan the Answer to Nigeria's Woes?", TIME, 2010-02-13. Retrieved on 2010-07-05. Archived from the original on 2010-05-14. 
  6. Tom Ashby, "Reclusive Yar'Adua wins ruling party ticket", Reuters (IOL), 17 Desemba 2006.
  7. "Attacks seek to derail Nigeria poll", Al Jazeera, 21 Aprili 2007.
  8. Punch Newspaper "NASS confirms Sambo as vice president" http://www.punchontheweb.com/Articl.aspx?theartic=Art201005185541038 Ilihifadhiwa 2 Oktoba 2011 kwenye Wayback Machine.
  9. Liberty News "National Assembly confirms Sambo as Vice President" http://www.myondostate.com/myondostate/newssend.php?id=203 Ilihifadhiwa 27 Aprili 2011 kwenye Wayback Machine.
  10. http://www.washingtonpost.com/world/violence-in-northern-nigeria-follows-goodluck-jonathans-election-win/2011/04/18/AFQ4jx1D_story.html Violence in northern Nigeria follows Goodluck Jonathan’s election win (Washington Post tar. 19-04-2011