Nenda kwa yaliyomo

Pythagoras

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kichwa cha sanamu ya Pythagorasi
Uhakiki wa Pythagorasi

Pythagoras (kwa Kigiriki Πυθαγόρας; mnamo 570 KK - baada ya mwaka 510 KK) alikuwa mtaalamu wa falsafa na hisabati wakati wa ustaarabu wa Ugiriki ya Kale.

Alizaliwa kisiwani Samos karibu na pwani ya Asia Ndogo.

Alipokuwa na umri wa miaka 14 alihamia Italia ya kusini iliyokuwa eneo lenye miji mingi ya Wagiriki wa Kale.

Pythagoras anakumbukwa hasa kwa "uhakiki wa Pythagoras" unaoeleza tabia za pembetatu mraba. Aligundua ya kwamba mraba juu ya hipotenusi (kiegana au upande kinyume cha pembe mraba) ni sawa na jumla ya miraba juu ya pande mbili nyingine.

Pythagorasi alianzisha kundi la kidini la wanahisabati; walitafuta siri za dunia katika namba wakiamini ya kwamba miungu walificha habari za dunia ndani ya namba zinazoonekana kote duniani kwa wataalamu wa hisabati hii takatifu.

Wanafunzi wake walifundisha uhamisho wa roho za watu kutoka mwili mmoja kwenda mwili mwingine; miili hufa, lakini roho zadumu. Pythagorasi alidai ya kwamba yeye alikumbuka maisha yake manne ya awali. Alikataa kuua wanyama kwa sababu aliona roho ndani ya wanyama pia, hivyo wanafunzi wake hawakula nyama.

Makala hii kuhusu mwanasayansi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Pythagoras kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.