Nenda kwa yaliyomo

Precision Air

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Precisionair Services)
Nembo ya Precision Air
Ndege ya shirika la precision nchini Tanzania

Precision Air ni kampuni ya ndege iliyo na makao yake jijini Dar Es Salaam nchini Tanzania. Inahudumia watalii na wafanyabiashara wanaosafiri kati ya viwanja vya ndege 10 nchini Tanzania, pamoja na ndege za kwenda nchi ya Kenya na Uganda.

Makao yake makuu ni kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, mjini Dar es Salaam na vituo viko kwenye viwanja vya ndege vya Kilimanjaro, Arusha na Mwanza.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Precision Air ilianzishwa mnamo 1991 na kuanza kutoa huduma mnamo 1994. Hapo awali, kampuni hii ilikuwa ya binafsi, lakini Kenya Airways ilinunua 49% kwa $ milioni 2, wiki chache tu baada ya South African Airways kununua 49% ya Air Tanzania. Asilimia 51 iliyobaki ni ya Michael Ngaleku Shirima.[1]

Kuanzia Oktoba 2011, Precision Air iliamua kuanza kuuza hisa zake katika soko la hisa la Dar es Salaam na hivyo umiliki wa Michael Shirima na Kenya Airways utapungua mpaka asilimia 33 kila mmoja.

Baada ya kuanza kuuza hisa zake kwa umma, Michael Shirima alitoa nusu ya hisa zake na Kenya Airways wakatoa nusu ya hisa zao. Kwa hivyo theluthi moja ya hisa hizo itamilikiwa na umma. Bei ya hisa moja inauzwa Shilingi 475.

Miji inayosafiria

[hariri | hariri chanzo]
Precision Air nchini Kenya.

Precision Air inasafiri hadi miji ya Dar es Salaam, Arusha, Kigoma, Kilimanjaro, Musoma, Mwanza, Bukoba, Shinyanga, Tabora, Zanzibar, Mombasa, Nairobi, Entebbe, Johannesburg na Hahaya

Mkakati wa kwenda katika maeneo mengine bado unaandaliwa.

Ndege zake

[hariri | hariri chanzo]

Hadi 26 Agosti 2009, Precision Air ilikuwa na ndege zifuatazo:

  • Ndege 4aina ya ATR42-400'
  • Ndege 5 aina ya ATR 72-500
  • Ndege 2 aina ya Boeing 737-300

Zilizowekwa oda

[hariri | hariri chanzo]
  • Ndege 2 aina ya ATR 42-500
  • Ndege 1 aina ya ATR 72-500
  • Majina ya ndege hizo ni 5HPAA,5HPAG,5HPWE na 5HPWF ambazo ni ATR42
  • Nyingine ni 5HPWA,5HPWB,5HPWC,5HPWD na 5HPWG ambazo ni ATR72
  • Vile vile wana BOEING 737-300 mbili ambazo ni 5HPAZ na 5HPMS

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]