Nenda kwa yaliyomo

Petro Nolasco

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtume Petro akimtokea Mt. Petro Nolasco; mchoro wa Francisco de Zurbarán, Museo del Prado, Madrid (Hispania.)

Petro Nolasco (kwa Kifaransa Pierre Nolasque; alizaliwa Mas-Saintes-Puelles, Ufaransa, 1189 hivi - Barcelona, leo nchini Hispania, 6 Mei 1256) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki anayekumbukwa hasa kwa juhudi zake za kukomboa Wakristo waliotekwa na Waislamu utumwani pamoja na kurudisha amani.

Kwa ajili hiyo alianzisha, pamoja na padri Raimundi wa Penyafort na mfalme Yakobo I wa Aragona, utawa wa Wamersedari naye mwenyewe mwaka 1245 huko Algiers alijitoa kutekwa kwa niaba yao akapigwa hata karibu kufa.

Alitangazwa mtakatifu na Papa Urbano VIII tarehe 30 Septemba 1628.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 6 Mei kila mwaka[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Martyrologium Romanum: ex Decreto Sacrosancti oecumenici Concilii Vaticani II instauratum auctoritate Ioannis Pauli P.P. II promulgatum, Romae 2001, ISBN 8820972107

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.