Nenda kwa yaliyomo

Paul Pogba

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Paul Pogba akicheza Manchester United.

Paul Labile Pogba (alizaliwa 15 Machi 1993) ni mchezaji wa soka wa Ufaransa ambaye anachezea klabu ya Serie A Juventus na timu ya taifa ya Ufaransa. Anafanya kazi kama kiungo wa kati, lakini anaweza kuwekwa kama winga wa kushoto, kiungo mkabaji, kiungo wa kujihami na mchezaji anayesogea mbele kutoka nyuma.[1]

Pogba alizaliwa Lagny-sur-Marne, Seine-et-Marne, kwa wazazi raia wa Guinea[2] . Yeye ni Mwislamu[3][4]. Ana kaka zake wawili ambao ni mapacha nao ni wacheza mpira wa miguu wa timu ya taifa ya Guinea[5].Florentin kwa sasa anacheza kama mlinzi wa ATK Mohun Bagan,[6] huku Mathias hivi karibuni akicheza kama mshambuliaji wa ASM Belfort.[6] Alipokuwa akikua, Pogba alikuwa shabiki wa Arsenal.[7]

Pogba alianza kazi yake ya mpira wa miguu akiwa na umri wa miaka sita akicheza huko Roissy-en-Brie, kilomita chache kutoka kusini mwa jiji lake. Alitumia misimu saba kuchezea Roissy-en-brie kabla ya kujiunga na Us Torcy, ambapo aliwahi kuwa nahodha wa timu ya watoto chini ya umri wa miaka 13. Baada ya msimu mmoja kuisha akiwa klabu ya Torcy, Pogba alijiunga na klabu ya wataalamu ya Le Havre. Katika msimu wake wa pili katika klabu hiyo, Pogba alikuwa nahodha katika timu na kuifikisha timu yake hadi fainali, Championnat National ya watoto wenye umri chini ya miaka 16 ikaipa ushindi timu ya Pogba ijulikanayo kama Le Havre na timu ya Pogba ikawa ya kimataifa kwa kupata ushindi.

Baada ya kuhamia Manchester United miaka miwili baadaye, mechi chache baadaye zilimshawishi kuondoka na kujiunga na Juventus ya Italia kwa uhamisho wa bure mwaka 2012, ambapo aliisaidia klabu hiyo kutwaa mataji manne mfululizo ya Serie A, mawili ya Coppa Italia na mawili ya Supercoppa Italiana. Wakati akiwa nchini Italia, Pogba alijidhihirisha zaidi kuwa mmoja wa wachezaji chipukizi wenye kutegemewa zaidi duniani na alipokea tuzo ya Golden Boy mwaka 2013, ikifuatiwa na Tuzo ya Bravo mwaka 2014.

Mwaka 2016, Pogba alitajwa kwenye Timu ya mwaka ya UEFA 2015 na 2015 FIFA FIFPro World XI baada ya kuisaidia Juventus kufika Fainali ya Ligi ya mabingwa ya UEFA 2015, ikiwa ni fainali yao ya kwanza katika kipindi cha miaka 12.

Uchezaji wa Pogba akiwa Juventus ulimfanya arejee Manchester United F.C. mwaka wa 2016 kwa ada ya uhamisho wa rekodi ya dunia wakati huo ya €105 milioni (£89.3 milioni).[8] Ada ndiyo iliyokuwa ya juu zaidi kulipwa na klabu ya Uingereza hadi 2021.[9] Katika msimu wake wa kwanza nyuma, alishinda Kombe la Ligi na Ligi ya Europa. Katika msimu wa 2018-19, alitajwa katika Timu ya Mwaka ya PFA.

Kimataifa, Pogba aliongoza Ufaransa kwa ushindi katika Kombe la Dunia la FIFA la U-20 2013 na kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora kwa uchezaji wake wakati wa mashindano. Alianza kuichezea timu ya waandamizi mwaka mmoja baadaye na kushiriki vyema katika Kombe la Dunia la FIFA la 2014, ambapo alitunukiwa Tuzo ya Mchezaji Bora Chipukizi kwa uchezaji wake. Baadaye aliwakilisha taifa lake kwenye UEFA Euro 2016 katika ardhi ya nyumbani, ambapo alimaliza kama mshindi wa pili, kabla ya kushinda Kombe la Dunia la FIFA la 2018, akifunga katika fainali.

  1. "Accueil". Guineefoot (kwa Kifaransa). Iliwekwa mnamo 2023-05-28.
  2. Fifield, Dominic (2014-07-03), "France's Paul Pogba: a complete midfielder worth 'two Gareth Bales'", The Guardian (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0261-3077, iliwekwa mnamo 2023-05-28
  3. Samuel, Henry (2016-10-12), "France has 'problem with Islam' and there is 'too much unwanted immigration', says Hollande in explosive book", The Telegraph (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0307-1235, iliwekwa mnamo 2023-05-28
  4. https://www.goal.com/en/news/1862/premier-league/2016/09/12/27358822/is-pogba-a-muslim-how-tall-is-ibrahimovic-your-manchester-united
  5. "Sparta Rotterdam heeft Pogba te strikken". Voetbalkrant.com (kwa Kiholanzi). 2016-08-31. Iliwekwa mnamo 2023-05-28.
  6. 6.0 6.1 "Paul Pogba's brother Florentin joins ATK Mohun Bagan on two-year deal", The Times of India, 2022-06-25, ISSN 0971-8257, iliwekwa mnamo 2023-05-28
  7. Liam Prenderville (2017-12-01). "Pogba explains why he was a fan of Arsenal growing up - and not Man United". mirror (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-05-28.
  8. https://football-italia.net/88963/official-pogba-signs-man-utd
  9. Sport, Telegraph (2016-08-09), "Paul Pogba completes Man Utd transfer for world-record fee", The Telegraph (kwa Kiingereza (Uingereza)), ISSN 0307-1235, iliwekwa mnamo 2023-05-28
Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Paul Pogba kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.