Panfilo na wenzake

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Panfilo na wenzake (walifia dini 16 Februari 309) ni kundi la Wakristo 12 waliouawa huko Kaisarea ya Palestina kwa ajili ya imani yao katika dhuluma ya kaisari Galerius Maksimianus.

Wa kwanza kuuawa walikuwa Wakristo 5 wa Misri: Elia, Yeremia, Isaya, Samweli na Danieli ambao waliteswa na hatimaye kuuawa kwa upanga.

Baada yao waliuawa padri Panfilo (mzaliwa wa Beirut, leo nchini Lebanoni), shemasi Valens wa Yerusalemu, Paulo wa Iamnia, Porfiri, Seleuko wa Kapadokia, Teodulo na hatimaye Juliani wa Kapadokia aliyechomwa moto taratibutaratibu.

Sifa yao imedumishwa na maandishi ya Eusebi wa Kaisarea, aliyekuwa mwanafunzi wa Panfilo na ameshuhudia pia utaalamu wake kuhusu Biblia.

Panfilo aliandika vitabu vitatu vya kumtetea Origen, lakini kimetufikia cha kwanza tu.

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini.

Sikukuu yao huadhimishwa tarehe ya kifo chao au tarehe 1 Juni[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]