Okavango

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mto wa Okavango
Feri juu ya mto Okavango nchini Botswana
Chanzo Nyanda za juu za Bié (Angola)
Mdomo Delta ya barani katika jangwa la Kalahari, Botswana
Nchi Angola, Namibia, Botswana
Urefu 1,600 km
Kimo cha chanzo 1,780 m
Mkondo 10,000,000,000 m³/mwaka (inaweza kukauka kwa muda)
Eneo la beseni 721.258 km²
Delta ya Ovango inavyoonekana kutoka angani

Okavango (pia: Okovango; katika Angola: Kubango au Cubango) ni mto wa Afrika ya kusini-magharibi. Inaanza nchini Angola katika milima ya Bié inapojulikana kwa jina la Kubango. Mwendo wake wa 1600 km ni kusini tu hadi jangwa la Kalahari inapoishia kwenye delta ya barani. Katika kusini ya Angola ni mpaka na Namibia. Inapita nchi ya Namibia mwanzoni wa kishoroba ya Caprivi na kuendelea Botswana inapoishia jangwani katika delta yake.

Jina la mto limepatikana kutoka kabila la Wakavango.

Chanzo cha mto ni kusini ya mji wa Vila Nova (Angola) katika milima ya Bié kwenye kimo cha 1,780 m. Mwanzoni mwendo wake ni ya haraka kuna maporomoko madogo. Halafu mto ni mpaka kati ya Angola na Namibia. Baada ya kupokea tawimto wa Kwito inaingia Namibia inapopita kanda nyembamba ya kishoroba ya Caprivi kwa kilomita chache. Kabla ya kuvuka mpaka wa Botswana mto unashuka mita 4 kwenye maporomoko ya Popa.

Takriban 70 km ndani ya Botswana mwendo wa mto unapanuka na kugawanyika kuwa delta ya barani yenye zaidi ya 16,000 km².

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

en: Okavango Basin (Watersheds of Africa)

Africa satellite plane.jpg Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Okavango kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.