Nenda kwa yaliyomo

Delta ya barani

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Tembo katika mabwawa wa delta ya Okavango
Delta ya Okavango jinsi inavyoonekana kutoka angani

Delta ya barani ni eneo nchini na mbali na bahari ambapo mto unapanuka kwa umbo la delta.

Kupanuka huku kunatokea kama mto unafika penye mtelemko mdogo kama tambarare au beseni. Kutokana na uhaba wa mtelemko kasi ya maji inapungua na mashapo yanatelemka chini yakijenga vizuizi na kusababisha kugawanyikiwa kwa mto kuwa na mikono mbalimbali.

Tofauti na delta ya mto baharini au ziwani delta ya aina hii hutokea barani kabisa.

Aina mbili za delta ya barani

[hariri | hariri chanzo]

Kimsingi kuna aina mbili za delta ya barani:

  • delta ya barani ambapo mto unaishia
  • delta ya barani ambapo mto unatoka tena na kuendelea.


Mto wa Okavango unakwisha baada ya kuvuka Afrika ya kusini magharibi kwa 1600 km katika jangwa la Kalahari (Botswana). Mikono ya delta na maziwa yamejenga mazingira yenye mimea na wanyama wengi katikati ya jangwa kubwa. Delta inavuta watalii wengi kila mwaka.

Mto unaendelea: Delta ya Niger

[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya ya kufika kwa mji wa Timbuktu mto Niger inapanuka kuwa delta. Pamoja na tawimto wa Bani delta hii iko katika beseni kubwa ya 40,000 km² inayoitwa Masina. Wakati wa mvua ziwa hujiitokeza lakini wakati wa ukame beseni ni eneo lenye mikono ya mto na mabwawa ya matope.

Kutoka hapa mto unatoka tena ukiendelea hadi Atlantiki.