Nyumbanitu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyumbanitu na msitu unaopatikana katika kijiji cha Mlevela, kata ya Mdandu, Wilaya ya Wanging'ombe, ni Km 15 kutoka Njombe mjini.

Jina "Nyumbanitu" ni muunganiko wa maneno mawili; nyumba na nitu. Neno "Nitu" manaa yake ni Giza au Nyeusi. Hivyo Nyumbanitu maana yake ni nyumba yenye giza au nyumba nyeusi.

Nyumbanitu si nyumba, kama lilivyo neno lenyewe, bali ni msitu mdogo, wenye ukubwa wa hekta mbili na nusu (2.5) tu, lakini una mambo ya kustaajabisha. Kuna watu ambao huenda Nyumbanitu kuomba mizimu iwape baraka katika mambo yao. Kuna ambao huenda kuchuma dawa, wengine huenda kujifunza mila na desturi za mahali hapo ambazo pengine zinahusiana na ushirikina n.k.

Vivutio vingine ni kama vile makaburi ya mashujaa wa Kibena, mawe ya ajabu, majengo ya kale ya Wajerumani, maporomoko ya maji ya Luhaji, mashamba makubwa ya chai n.k.

Marejeo ya Nje[hariri | hariri chanzo]


Tovuti za nje[hariri | hariri chanzo]

Filamu kuhusu Nyumbanitu kwenye Youtube,imeangaliwa April 2018

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Nyumbanitu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.