Nyigu mlanyuki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Nyigu mlanyuki
Philanthus triangulum akibeba nyuki aliyepooza
Philanthus triangulum akibeba nyuki aliyepooza
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba)
Familia ya juu: Apoidea
Familia: Crabronidae
Jenasi: Philanthus
Fabricius, 1790
Ngazi za chini

Spishi 135, 11 katika Afrika ya Mashariki;

Nyigu walanyuki ni nyigu wa ukubwa wa kati wa jenasi Philanthus katika familia Philanthidae na familia ya juu Apoidea katika oda Hymenoptera ambao huwinda nyuki (nyigu wengine pia kwa spishi kadhaa) ili kutaga mayai juu yao. Wanatokea duniani kote isipokuwa Australia, Amerika ya Kusini na Antakitiki. Kwenye mawili ya kwanza spishi nyingine za nyigu zinajaza nafasi ya kukamata nyuki, kama jenasi Trachypus katika Amerika ya Kusini. Kwa jumla Philanthus ina spishi 137 na 11 zinapatakana Afrika ya Mashariki.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Nyigu walanyuki ni nyigu kubwa kiasi wenye urefu wa mm 10-18. Kwa ujumla huwa na rangi ya nyeusi na milia njano, ambayo inaweza kuwa pana sana, na uso wa njano. Vinginevyo, fumbatio inaweza kuwa njano kabisa. Kichwa ni kipana chenye macho makubwa. Kwa nyingine, nyigu hawa hawana sifa maalum.

Biolojia[hariri | hariri chanzo]

Spishi nyingi za jenasi Philanthus hutumia nyuki kama mbuawa, ambao hutumika kama chakula cha mabuu yao. Mara nyingi hubobea katika spishi moja, kama vile nyuki-asali kwa kisa cha nyigu mlanyuki wa Ulaya (Philanthus triangulum), lakini wengine huwinda spishi nyingi tofauti. Wengine hata huwinda Hymenoptera nyingine, ambayo inaweza kujumuisha spishi yao yenyewe[1]. Wapevu hula [[mbochi,] Wanajulikana kwa kuchoma mbuawa wao katika eneo la kiwmbo juu ya uso wa tumbo, ambapo sumu inapooza haraka misuli kuu ya hiari, lakini haiui mbuawa. Mbuawa anaweza kujaribu kuchoma kwa kurudi, lakini daima hunyakuliwa kwa njia ambayo sehemu tu za silaha za mwili wa nyigu zinawasilishwa. Nyigu mlanyuki hubeba mbuawa wake kwenye handaki, lakini kwa kawaida humhifadhi kwa muda mfupi tu, hadi atumike baadaye kuandaa shimo la seli, ambapo yai hutagwa[1].

Handaki ya nyigu mlanyuki wa Ulaya inaweza kuwa na urefu wa mita 1. Sehemu ya kwanza ya handaki inateremka chini kwa pembe ya 30°, baada ya hapo inakuwa na usawa. Hadi handaki 34 za kando, kila moja ikiishia kwenye chumba cha kizazi, hutengana na handaki kuu. Kila chumba cha kizazi kinapata akiba ya nyuki mmoja hadi sita[1]. Mashimo ya kiota ya spishi nyingine ni mafupi zaidi na yana muundo tofauti.

Spishi za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

  • Philanthus adamsoni
  • Philanthus amabilis
  • Philanthus basilewskyi
  • Philanthus bredoi
  • Philanthus capensis
  • Philanthus flagellarius
  • Philanthus limatus
  • Philanthus loeflingi
  • Philanthus nigrohirtus
  • Philanthus pilifrons
  • Philanthus triangulum

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 {{cite book | last = Piper | first = Ross | title = Extraordinary Animals: An Encyclopedia of Curious and Unusual Animals