Nenda kwa yaliyomo

Nyamagoma

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Nyamagoma ni kata ya Wilaya ya Ngara katika Mkoa wa Kagera, Tanzania yenye msimbo wa posta namba 35721 [1].

Kata ya Nyamagoma inaundwa na jumla ya vijiji vitatu ambavyo ni Murubanga, Kititiza na Kumubuga, ambavyo vina jumla ya vitongoji 13 kwa mtiririko ufuatao:

1. Murubanga (7) (i) Murubanga (ii) Kahama (iii) Mukitoma (iv) Mtakuja (v) Mpimba (vi) Mumbizi (vii) Mulonzi

2. Kititiza (3) (i) Kititiza (ii) Kukabaho (iii) Nyaruhanga

3. Kumubuga (3) (i) Songambele (ii) Bichibo (iii) Murumono

Wakati wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022, idadi ya wakazi wa kata ilikuwa watu 10,112 ikijumuisha wanawake 5,273 na wanaume 4,839 [2]. Wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, idadi ya wakazi wa kata ilikadiriwa kuwa watu 7,178.[3]

Makabila yanayopatikana ndani ya kata ya Nyamagoma ni Washubi, Wasukuma, Wasubi, Wasubwa, na Wahaya. Wakazi wa kata hiyo ni wakarimu sana. Aidha katika kuangazia utamaduni wa wakazi wa kata ya Nyamagoma, uwepo wa makabila mchanganyiko, pamoja na mifumo tofauti ya maisha, vinavutia sana.

Shughuli kubwa za kiuchumi katika kata hiyo ni kilimo na ufugaji.

Kata za Wilaya ya Ngara - Mkoa wa Kagera - Tanzania

Bugarama | Bukiriro | Kabanga | Kanazi | Kasulo | Keza | Kibimba | Kibogora | Kirushya | Mabawe | Mbuba | Muganza | Mugoma | Murukurazo | Murusagamba | Ngara Mjini | Ntobeye | Nyakisasa | Nyamagoma | Nyamiaga | Rulenge | Rusumo

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kagera bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Nyamagoma kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.