Nona

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Nona wa Nazianzo (305 hivi - 374 hivi) alikuwa mke wa Gregori Mzee na mama wa Gregori wa Nazianzo, Sesari wa Nazianzo na Gorgonia. Aliishi huko Kapadokia, mkoa wa Dola la Roma katikati ya Uturuki wa leo.

Tangu kale anaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama mtakatifu pamoja na familia yake yote.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 5 Agosti.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kuolewa , Nona alimsaidia Gregori mumewe kuongokea Ukristo kutoka madhehebu yenye mchanganyiko wa Uyahudi na Upagani yaliyomuabudu Hypsistos, Mungu "Aliye Juu".

Aliishi mpaka baada ya kifo cha mumewe, aliyefikia uaskofu, na ya wanae wawili.[1]

Mwanae maarufu zaidi, Gregori, ambaye pia alifikia uaskofu na anaheshimiwa kama mwalimu wa Kanisa, alitangaza sifa za mamaye[2]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Jones, Terry. Nonna. Patron Saints Index. Iliwekwa mnamo 2007-05-06.
  2. My mother was a worthy companion for such a man [as my father] and her qualities were as great as his. She came from a pious family, but was even more pious than they. Though in her body she was but a woman, in her spirit she was above all men... Her mouth knew nothing but the truth, but in her modesty she was silent about those deeds which brought her glory. She was guided by the fear of God...Rabenstein, Katherine (August 1998). Nonna of Nazianzen, Matron. Saints O' the Day for August 5. Jalada kutoka ya awali juu ya February 6, 2007. Iliwekwa mnamo 2012-02-23.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]