Nenda kwa yaliyomo

Noeli Chabanel

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wajesuiti wafiadini wa Amerika Kaskazini.

Noeli Chabanel, S.J. (Saugues, Ufaransa 2 Februari 1613Midland, Ontario, Kanada, 8 Desemba 1649) alikuwa padri wa Wajesuiti mmisionari kwa Wahuroni wa Amerika Kaskazini tangu mwaka 1643[1]

Alikuwa amemwekea Mungu nadhiri ya kubaki katika misheni hiyo pendwa hadi kifo chake. Akiwa anakimbia shambulio la Wairoki, kabila lingine la Waindio, waliomuua mwenzake Charles Garnier[2], akiwa msituni na mtu aliyeasi dini, aliuawa naye kwa chuki dhidi ya imani [3].

Alitangazwa na Papa Pius XI kuwa mwenye heri tarehe 21 Juni 1925, na kuwa mtakatifu tarehe 29 Juni 1930.

Sikukuu ya kundi lake la wafiadini huadhimishwa tarehe 19 Oktoba, lakini ya kwake mwenyewe huadhimishwa tarehe ya kifodini chake[4].

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. [1]
  2. Gray, Charlotte; Angel, Sara (2004). The Museum Called Canada: 25 Rooms of Wonder. Random House Canada. ISBN 978-0-679-31220-8.
  3. http://www.santiebeati.it/dettaglio/92994
  4. Martyrologium Romanum
  • (Kifaransa) Rochemonteix, Les Jésuites et la Nouvelle-France au XVIIe siècle, I, 97–100, 409–18.
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.