Nikola Owen

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Nikola katika mateso.

Nikola Owen, S.J. (Oxford, 1560 hivi – London, 22 Machi 1606) alikuwa bradha Mjesuiti aliyesaidia sana kudumisha imani Katoliki nchini Uingereza [1].

Alitangazwa mwenye heri na Papa Pius XI mwaka 1929 na mtakatifu mwaka 1976 na Papa Paulo VI.

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe ya kifodini chake[2].

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Baada ya kulemaa mguu, kwa miaka mingi alifanya kazi ya kusaidia na kuficha [3][4] mapadri waliofanya utume nchini bila kujali dhuluma ya serikali, wakiwemo ndugu zake wawili [5] na Edmundi Campion[6]. Kwa ajili hiyo aliwahi kufungwa na kuteswa (1581 na 1594)[7].

Alijiunga na Wajesuiti mwaka 1597 akaendelea na huduma zake muhimu hadi alipokamatwa[8][9] na kuteswa kikatili kwa siku kadhaa na hatimaye kuchanwa vipandevipande chini ya mfalme James I[10].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. In Narrative of the Gunpowder Plot, Fr. John Gerard, S.J. wrote of him: I verily think no man can be said to have done more good of all those who laboured in the English vineyard. He was the immediate occasion of saving the lives of many hundreds of persons, both ecclesiastical and secular.
  2. Martyrologium Romanum
  3. "Mar. 22, St. Nicholas Owen, S.J., Martyr", National Catholic Reporter, 2010-03-22. (en) 
  4. "Nicholas Owen SJ | Jesuits in Britain". www.jesuit.org.uk (kwa Kiingereza). Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2021-03-23. Iliwekwa mnamo 2018-08-24.  More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)
  5. "We can learn a lot from St Nicholas Owen, the priest-hole maker | CatholicHerald.co.uk", CatholicHerald.co.uk, 2014-08-25. Retrieved on 2021-03-19. (en-US) Archived from the original on 2018-08-24. 
  6. "The Jesuit Curia in Rome". www.sjweb.info. Iliwekwa mnamo 2018-08-24. 
  7.  "Nicholas Owen". Catholic Encyclopedia. New York: Robert Appleton Company. 1913.
  8. Lives of the Saints By Alban Butler, Peter Doyle, ISBN 0-86012-253-0
  9. Realising just whom they had caught, and his value, Secretary of State Robert Cecil, 1st Earl of Salisbury exulted: "It is incredible, how great was the joy caused by his arrest... knowing the great skill of Owen in constructing hiding places, and the innumerable quantity of dark holes which he had schemed for hiding priests all through England".
  10. http://www.santiebeati.it/dettaglio/93218
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.