Nikandro na Marsiano

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kikanisa cha Wat. Nikandro, Marsiano na Daria huko San Nicandro Garganico, Italia.

Nikandro na Marsiano (walifariki Venafro, Molise, Italia, 17 Juni 303) walikuwa Wakristo waliouawa kutokana na imani yao wakati wa dhuluma ya kaisari Diokletian wa Dola la Roma.

Kabla ya kuongokea Ukristo walikuwa askari, labda kutoka Mesia, katika Bulgaria ya leo, lakini hawakusita kukabili kifo ili wajiunge na dini hiyo. Kaisari alipotoa tuzo kwa jeshi, waliikataa pamoja na agizo la kutoa sadaka kwa miungu [1].

Tangu kale wanaheshimiwa na Wakatoliki na Waorthodoksi kama watakatifu wafiadini, pengine pamoja na Daria anayesemekana alikuwa mke wa Nikandro akauawa siku chache baada yao kwa sababu ya kumchochea mumewe asikane imani yao mpya.

Sikukuu yao ni tarehe 17 Juni[2].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.