Mwanamuziki
Mwanamuziki ni mtu anayepiga vyombo vya muziki kama vile gitaa au piano au mtu mwenye kuimba.
Mwanamuziki ni mtu anayetunga muziki, hata kama anaandika nyimbo kwa ajili ya kupigwa na watu wengine. Mtu anayetunga nyimbo anaitwa mtunzi. Kawaida mtunzi huwa haimbi, lakini kuna kipindi mtunzi naye huwa anaimba japokuwa yeye ni mtunzi.
Hapa kuna orodha chache ya wanamuziki maarufu duniani:
- Johann Sebastian Bach (Mtunzi)
- Ludwig van Beethoven (Mtunzi)
- Wolfgang Amadeus Mozart (Mtunzi)
- Duke Ellington (Mtunzi, na apiga piano)
- Bob Marley (Anapiga gitaa la umeme, na anaimba)
- Paul McCartney (Mwimbaji, anapiga besi na gitaa)
- Michael Jackson (Mwimbaji)
- Jimi Hendrix (Anapiga gitaa la umeme, pia anaimba)
- Ali Khan (Mwimbaji, na apiga sitaa)
- Cat Stevens (mwimbaji)
- Wei Wei (Mwimbaji)
Mwanamuziki pia anaweza kuunda kundi la muziki na kuweza kuimba nao pamoja. Kama kundi la muziki lina watu wengi wanaopiga vyombo vya muziki kwa pamoja, kama vile muziki wa kina Beethoven, basi inaitwa orchestra. Na kama watu wengi wanaimba, kama jinsi inayokuwa katika kanisa, hiyo inaitwa kwaya. Na kama watu wachache tu wanaimba na kutumia viyombo kadhaa, basi hao wanaitwa bendi. Kuna kipindi hata bendi nayo huwa na jina sawa tu na lile la mwimbaji.
Hapa kuna orodha chache ya mabendi maarufu duniani:
Na hapa kuna orodha tena ya orchestra mashuhuri duniani:
- The London Symphony Orchestra, Uingereza
- The New York Philharmonic Orchestra, Marekani
- The Berlin Philharmonic Orchestra, Ujerumani
- The Belgrade Philharmonic Orchestra, Serbia
Makala hii kuhusu mambo ya muziki bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mwanamuziki kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |