Nenda kwa yaliyomo

Belgrad

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Belgrade)
Bendera ya Belgrad

Belgrad (Kiserbia: Београд - beograd "mji mweupe") ni mji mkuu wa Serbia. Iko kando la mto Danube mahali ambako mto Sava unapoishia humo. Ni pia mji mkubwa wa nchi mwenye wakazi 1,710,000 (mwaka 2002).

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Mji umejulikana tangu zamani za Dola la Roma kwa jina Singidun ulipokuwa mji wa kikelti. Waroma walijenga mji wa kiroma palepale kwa jina la Singidunum. Tangu kufika kwa Waslavoni mji ulipata jina "mji mweupe" au "boma nyeupe" kwa lugha mbalimbali.

Belgraf ilitawaliwa na nchi mbalimbali kama vile Bulgaria, Bizanti na Hungaria. Serbia ilianza kuenea hadi shemu hizi tangu karne ya 13. Mwaka 1403 ilitangazwa na Stefan Lazarević (1389-1427) kuwwa mji mkuu wa Serbia ambayo wakati ule ilisukumwa kaskazini kutokana na mashambulio ya Waosmani.

Tangu mwaka 1521 Belgrad ilivamiwa na Waturuki walioendelea kuitawala hadi karne ya 19 hata kama mju ulikuwa mahali pa mapigano mengi kati ya Uturuki na Austria ikatwaliwa na kupotelewa na Austria mara tatu katika karne zile.

1817 ilikuwa mji mkuu wa Utemi ya Serbia iliyofufuka tena. Imebaki hivyo hadi leo. Wakati ambako Serbia ilikuwa sehemu ya Yugoslavia ilikuwa pia mji mkuu wa Yugoslavia.

Picha za Belgrad

[hariri | hariri chanzo]
Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Belgrad kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.