Mugirango Kaskazini

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mugirango Kaskazinini moja ya Majimbo ya Uchaguzi ya Kenya linalopatikana katika Wilaya ya Nyamira, mkoani Nyanza. Mbunge wa jimbo hili ni Wilfred Moriasi Ombui[1]. Alikishinda kiti hiki katika Uchaguzi wa 2007 huku akimshinda mpinzani wake Godfrey Masanya Okeri ambaye ndiye aliyekuwa Mbunge kati ya 2002 na 2007[2].

Idadi ya Wapiga Kura[hariri | hariri chanzo]

Mnamo 1999, Jimbo hili lilikuwa na jumla ya watu 156,344, 89092 kati yao wakiwa wamejiandikisha kupiga kura mnamo 2007[3]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Awali, eneo la Mugirango Kaskazini lilikuwa eneo moja kubwa. Mnamo 1966, jimbo hili liligawanya na kuwa Mugirango Magharibi na Mugirango Kaskazini iliyopungua. Jina lake lilibadilishwa mnamo 1974 na kuwa Borabu / Mugirango Kaskazini, ambalo mwishowe lilibadilishwa kuwa Mugirango Kaskazini / Borabu mnamo 1986.[3]

Wadi za Kupiga Kura[hariri | hariri chanzo]

Wodi ziundazo Mugirango Kaskazini ni: Ekerenyo, North Mugirango Chache, Bomwagamo, Kiabonyoru, Kiangeni, Makenene, Nyansiongo na Esise.

Tazama Pia[hariri | hariri chanzo]

Virejeleo[hariri | hariri chanzo]

  1. Maendeleo Afrika,www.afdevinfo.com
  2. Ripoti ya Maendeleo ya Afrika www.afdevinfo.org
  3. 3.0 3.1 Mukhtasari wa Ripoti ya Majimbo ya Ubunge; www.kenyaelections.com

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]