Nenda kwa yaliyomo

Wilfred Moriasi Ombui

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Wilfred Ombui Moriasi

Wilfred Ombui Moriasi ni mwanasiasa wa Kenya, mwanachama wa Chama cha KANU. Miaka 2009-2013 alikuwa mbunge akiwakilisha eneo bunge la Mugirango Kaskazini kwa tikiti ya Chama cha KANU[1]

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Ombui alizaliwa katika kijiji cha Bonyunyu karibu na Kenyoro, Kata ya Itibo, Tarafa ya Ekerenyo, Wilaya ya Nyamira Mkoa wa Nyanza nchini Kenya

Alisoma katika Shule ya Msingi ya ELCK Kenyoro kabla ya kujiunga na Shule ya Upili ya Kisii.

Kazi zingine

[hariri | hariri chanzo]

Kando na kuwa mwalimu wa Shule ya Msingi, Ombui pia anajulikana na wengi kwa kuwa meneja wa Chama cha walimu cha Mwalimu SACCOS tawi la Gusii kwa muda Mrefu.

Alijitosa ulingoni mwa siasa kwa mara ya kwanza wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu wa 2007. Umaarufu wake ulizambaa haraka na akakishinda kiti hicho cha Ubunge huku akiwashinda wapinzani wake akiwemo mtangulizi wake Godfrey Okeri Masanya na Mwanasheria Joseph Kiangoi Ombasa.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
Alitanguliwa na
Godfrey Masanya Okeri
Mbunge wa Mugirango Kaskazini
2007-
Akafuatiwa na
_
  1. Members Of The 10th Parliament Ilihifadhiwa 16 Juni 2008 kwenye Wayback Machine.. Bunge la Kenya. Accessed 19 Juni 2008.