Nenda kwa yaliyomo

Mto Zhu Jiang

Majiranukta: 22°46′N 113°38′E / 22.767°N 113.633°E / 22.767; 113.633
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

22°46′N 113°38′E / 22.767°N 113.633°E / 22.767; 113.633


Mto Zhu Jiang (Pearl River)
Beseni ya Zhu Jiang
Chanzo (vyanzo tofauti)
Mdomo Bahari ya Kusini ya China
Nchi China
Urefu km 2,400
Kimo cha chanzo m
Tawimito upande wa kulia Xi Jiang na Bei Jiang
Tawimito upande wa kushoto Dong Jiang
Mkondo m3 9,500
Eneo la beseni km2 453,700
Miji mikubwa kando lake Guangzhou, Dongguan, Shenzhen, Zhongshan, Zhuhai, Macau, Hongkong

Mto Zhu Jiang (kwa Kiingereza: Pearl River, "mto wa Lulu", zamani ilijulikana pia kama Canton River) ni jina la delta kubwa ya mito mbalimbali inayoishia kwenye Bahari ya China Kusini, na pia jina la pamoja kwa mfumo wa mito inayoungana hapa. Mito hiyo hujulikana kama mito ya Xi ("Magharibi"), Bei ("Kaskazini"), na Dong ("Mashariki") katika jimbo la Guangdong.

Kuanzia chanzo cha mto Xi, mfumo wote wa Zhu Jiang huwa na urefu wa km 2,400. Kwa hiyo ni mto mrefu wa tatu wa China baada ya Mto Yangtze na Mto Njano. Kufuatana na mkondo wa maji unayobeba ni mto mkubwa wa pili baada ya Yangtze. Jumla ya beseni lake ni km2 409,480. Beseni hilo linapokea pia maji kutoka kaskazini mwa Vietnam.

Mdomo wa mto Zhu Jiang ni kama hori ya bahari. Kabla yake liko jiji la Guangzhou. Hori ya mwisho inatenganisha Macau na Zhuhai upande wa magharibi na Hong Kong pamoja na Shenzhen upande wa mashariki.

Tawimito

[hariri | hariri chanzo]
  • Bei (北江)
  • Dong (东江)
  • Xi (西江)
    • Yu (鬱江)
      • Yong (邕江)
        • Zuo (左江)
        • You (右江)
    • Xun (浔江)
      • Qiang (黔江)
      • Liu (柳江)
        • Rong(融江)
        • Hongshui (红水河)
          • Beipan (北盘江)
          • Nanpan (南盘江)
            • Ba (灞水 or 灞河)
    • Gui (桂江)
      • Li (漓江)
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mto Zhu Jiang kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.