Yangtze (mto)
Chanzo | Tibet (China) |
Mdomo | Bahari ya Mashariki ya China karibu na Shanghai |
Nchi | China |
Urefu | 6,380 km |
Kimo cha chanzo | 5,405 m |
Mkondo | 31,900 m³/s |
Eneo la beseni | 1,800,000 km² |
Miji mikubwa kando lake | Chongqing, Wuhan, Nanjing, Shanghai |
Mto Yangtze (pia: Changjiang) ni mto mkubwa nchini China na pia mto mrefu wa Asia yote. Duniani huhesabiwa kama mto mrefu wa tatu baada ya Amazonas na Naili).
Mwendo wake wote wa kilomita 6,300 pamoja na kilomita 2,800 zinazotumiwa na meli uko ndani ya China.
Chanzo chake iko katika nyanda za juu za Tibet. Inafuata mwelekeo wa kusini-mashariki hadi kilomita 1,500 baada ya chanzo. Hapa inasimamishwa na milima yenye mawe magumu na kugeuka ikuelekea sasa kwenda kaskazini-mashariki.
Katikati ya mwendo wake mto hupita kwenye mabode makali. Hapa serikali ya China iliamua kujenga lambo la magenge matatu linalo umbara zake zimeonakana kwa sababu watu milioni 1.5 walipaswa kuhamishwa na tayari tatizo la matope kujaza ziwa nyuma ya lambo limeshaanza.
Kuna miji mingi mikubwa inayotegemea mto huu na machafuko kutoka ya viwanda vyao yamekuwa tatizo.
Katika historia mwendo wa Yangtze ilikuwa mpaka kati ya China ya kaskazini na China ya kusini.
Makala hii kuhusu maeneo ya China bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Yangtze (mto) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |