Mohammed Gulam Dewji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Mohamed Gulam Dewji)
Jump to navigation Jump to search
Dewji mwaka 2013.

Mohammed Gulam Dewji (amezaliwa tarehe 8 Mei 1975) ni mwekezaji na mfanyabiashara nchini Tanzania aliyewahi kuwa pia mbunge katika Bunge la Tanzania miaka 2005-2015.

Raisi mstaafu wa Tanzania, Mh. Jakaya Kikwete na Mohammed Dewji katika kampeni za uchaguzi za mwaka 2010.

Ukiachana na uanasiasa, ni miongoni mwa watu matajiri zaidi Afrika; kwa Tanzania ni wa kwanza katika utajiri.

Ana utajiri wa dola za Marekani bilioni 1.3 unaomfanya ashike nafasi ya 1,500 duniani na ya 31 barani Afrika, mwaka 2015.

Mwaka 2017 jarida maarufu duniani la Forbes lilimtaja kuwa tajiri wa 17 barani Afrika.

Kutekwa[hariri | hariri chanzo]

Tarehe 11 Oktoba 2018, saa 11:35 alfajiri, Dewji alitekwa na watu wenye silaha, nje ya Colosseum Hotel mjini Dar es Salaam, alipokwenda kufanya mazoezi.

Tarehe 15 Oktoba familia ilitangaza kuwa tayari kutoa shilingi bilioni moja kwa atakayetoa taarifa itakayosaidia kumpata hai mtoto wao.

Tarehe 20 Oktoba saa 8 usiku Dewji aliachwa huru katikati ya jiji la Dar es Salaam na watu wasiojulikana waliotumia gari lilelile lililotumika kumteka[1].

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]