Nenda kwa yaliyomo

Mkunga Mfyonzaji

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkunga mfyonzaji
Mkunga mfyonzaji wa bahari (Petromyzon marinus)
Mkunga mfyonzaji wa bahari (Petromyzon marinus)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Nusufaila: Vertebrata (Wanyama wenye uti wa mgongo)
Ngeli ya juu: Cyclostomata
Ngeli: Hyperoartia
Oda: Petromyzontiformes
Ngazi za chini

Familia 3:

Kinywa cha mkunga mfyonzaji wa bahari, Petromyzon marinus

Mikunga wafyonzaji ni wanyama wa oda Petromyzontiformes katika ngeli Hyperoartia wanaofanana na mikunga wa kawaida lakini ni wanyama tofauti sana. Wao ni ukoo wa kale wa samaki bila mataya. Mkunga mfyonzaji aliyekomaa anaweza kuainishwa kwa kuwa na kinywa cha kufyonzia kwa umbo wa mpare kilicho na meno makali. Pamoja na mikunga-ute (ngeli Myxini) wanaunda ngeli ya juu Cyclostomata (maana: wenye kinywa cha mviringo).

Kuna spishi 18 za mikunga wafyonzaji zilizopo. Spishi hizi ni vidusia waladamu na hula kwa kuchochea ndani ya mwili wa samaki wengine ili kufyonza damu yao[1]. Spishi 9 baina hizi huhamia kutoka kwa maji ya chumvi hadi maji baridi ili kuzaliana (baadhi yao pia wana idadi za maji baridi) na tisa wanaishi katika maji baridi tu. Katika ngeli Hyperoartia kuna spishi 20 nyingine zisizofyonza damu na hizi ni spishi za maji baridi[2]. Waliokomaa wa spishi hizi hawali; wanaishi wakila akiba waliyopata kwa njia ya kuchuja chakula kutoka maji wakati walikuwapo lava au amoseti (Kiing. ammocoetes).

Msambazo

[hariri | hariri chanzo]

Mikunga wafyonzaji huishi zaidi katika maji ya pwani, ingawa spishi kadhaa (k.m. Geotria australis, Petromyzon marinus na Entosphenus tridentatus) husafiri umbali mkubwa kiasi katika bahari wazi[3] kama inavyothibitishwa na ukosefu wao wa kutengwa kwa uzazi kati ya idadi. Spishi kadhaa hupatikana katika maziwa yaliyozungukwa kwa ardhi. Hupatikana katika maeneo mengi ya wastani lakini hawatokei katika Afrika. Lava zao (amoseti) zina uvumilivu mdogo kwa maji ya joto kiasi, ambalo linaweza kueleza kwa nini hawasambawi katika kanda za tropiki.

Mofolojia

[hariri | hariri chanzo]

Waliokomaa hufanana kijuujuu na mikunga kwa kuwa wana mwili mrefu bila magamba na huweza kuwa na urefu wa sm 13-100. Mikunga wafyonzaji waliokomaa wana macho makubwa, tundu moja la pua juu ya kichwa na matundu saba ya matamvua kila upande wa kichwa, lakini wanakosa jozi za mapezi. Koromeo limegawanyika, sehemu ya chini ikiunda neli ya kupumua ambayo imetengewa kinywa kwa vali inayoitwa velo ([[Kiing. velum).

Tabia za kipekee za kimofolojia za mikunga wafyonzaji, kama vile kiunzo chao cha gegedu, huonyesha kuwa ni kundi la dada la vertebrata wote walio na mataya (Gnathostomata). Mara nyingi huchukuliwa kama kundi la msingi la vertebrata[4] . Badala ya pingili za uti wa mgongo za kweli wana mfululizo wa miundo ya gegedu inayoitwa arkualio iliyopangwa hapo juu ya ugwe wa neva.

  1. Hardisty, M. W.; Potter, I. C. (1971). Hardisty, M. W.; Potter, I. C. (whr.). The Biology of Lampreys (toleo la 1). Academic Press. ISBN 9780123248015.
  2. DOCKER, Margaret F (2006). "Bill Beamish's Contributions to Lamprey Research and Recent Advances in the Field". Guelph Ichthyology Reviews. 7. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 27 Agosti 2014. Iliwekwa mnamo 12 Juni 2014. {{cite journal}}: Unknown parameter |= ignored (help); Unknown parameter |deadurl= ignored (|url-status= suggested) (help)
  3. Silva, S.; Araújo, M. J.; Bao, M.; Mucientes, G.; Cobo, F. (2014). "The haematophagous feeding stage of anadromous populations of sea lamprey Petromyzon marinus: low host selectivity and wide range of habitats". Hydrobiologia. 734 (1): 187–199. doi:10.1007/s10750-014-1879-4.
  4. MicroRNAs reveal the interrelationships of hagfish, lampreys, and gnathostomes and the nature of the ancestral vertebrate

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]