Nenda kwa yaliyomo

Mkoa wa Kasai Mashariki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Mkoa wa Kasai Mashariki
Mahali paMkoa wa Kasai Mashariki
Mahali paMkoa wa Kasai Mashariki
Nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Makao makuu Mbuji-Mayi
Serikali
 - Gavana Dominique Nkangu Kabengela
Idadi ya wakazi (2005 est.)
 - Wakazi kwa ujumla 7,100,000
National language Tshiluba
Tovuti:  kasaiest.cd

Kasai Mashariki (Kasai-Oriental kwa Kifaransa) ni moja ya mikoa 11 ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Inapakana na mikoa ya Kasai Magharibi upande wa magharibi, Équateur upande wa kaskazini, Orientale upande wa kaskazini mashariki, Maniema upande wa mashariki na Katanga upande wa kusini. Kasai-Oriental ni kati ya maeneo duniani penye almasi nyingi. Makao makuu ya mkoa ni Mbuji-Mayi.

Jina la mkoa latokana na mto Kasai.

Historia

[hariri | hariri chanzo]

Kasai-Oriental inakaliwa hasa na Waluba. Kabla ya ukoloni sehemu kubwa za mkoa zilkuwa chini ya milki ya Luba.

Wakati wa uhuru wa Kongo wanasiasa wa sehemu hii walijaribu kuanzisha dola la kujitegema ya Kasai kusini lakini jeshi la serikali kuu ilivamia eneo lake. Baada ya vita ya miezi minne iliyokuwa na wahanga maelfu eneo lilirudishwa Kongo na kugawiwa.

Eneo la mji wa Mbuji-Mayi linazalisha asilimia 10 ya almasi zote zinazotolewa duniani. Uchimbaji unasimamiwa na kampuni ya Société Minière de Bakwanga. Wananchi wengine wanajaribu kuchimba almasi kibinafsi. Kwa jumla wakazi wa mkoa hawafaidiki na utajiri huu.

Kifaransa ni lugha rasmi. Tshiluba ni lugha inayotumiwa na wakazi wengi ambacho ni moja ya lugha za kitaifa za Kongo.




 
Mikoa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Bandera Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Équateur | Ituri | Kasai | Kasai Mashariki | Katanga Juu | Kinshasa | Kivu Kaskazini | Kivu Kusini | Kongo Kati | Kwango | Kwilu | Lomami | Lomami Juu | Lualaba | Lulua | Mai-Ndombe | Maniema | Mongala | Sankuru | Tanganyika | Tshopo | Tshuapa | Ubangi Kaskazini | Ubangi Kusini | Wele Chini | Wele Juu
+/-