Mkoa wa Équateur

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mkoa wa Ikweta
Ekwatéli / Équateur
Mahali pa Mkoa wa Équateur katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Mahali pa Mkoa wa Équateur katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Viwianishi: 00°04′N 18°16′E / 0.067°N 18.267°E / 0.067; 18.267
Nchi Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Wilaya 7
Mji mkuu Mbandaka
Serikali
 - Gouverneur
Eneo
 - Mkoa 103,902 km²
Idadi ya wakazi (1998)
 - 1,626,606

Mkoa wa Équateur (Mkoa wa Ikweta) ni moja ya mikoa 26 ya kujitawala ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Idadi ya wakazi wake ni takriban 1,626,606. Mji mkuu ni Mbandaka.

Mkoa huu ulianzishwa kutokana na ugawaji mpya wa katiba ya Kongo ya 2005. Kabla ilikuwa sehemu ya jimbo la Equateur pamoja na mikoa ya sasa Ubangi-Kaskazini, Mongala, Ubangi-Kusini na Tshuapa. Kabla ya kuingizwa katika jimbo la Equateur wakati wa rais Mobutu Sese Seko iliwahi kuwa mkoa wa pekee kati ya 1962-1966 kwa jina la Cuvette-Centrale.

Eeno la mkoa huu uko katika kaskazini-magharibi ya Kongo kando la mto Kongo. Upande wa magharibi unapakana na Kongo-Brazzaville.

Sehemu kubwa ya Hifadhi ya taifa ya Lomako Yokokala iko ndani ya mkoa huu. Hifadhi hii inajulikana hasa kwa sababu hapa iko mahali pa pekee duniani wanapoishi nyani kubwa wa Bonobo wanaohesabiwa kati ya hominidi.

Picha za Équateur[hariri | hariri chanzo]


Flag-map of the Democratic Republic of the Congo.svg Makala hii kuhusu maeneo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Mkoa wa Équateur kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.


WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: 
Mikoa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Bandera Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
Équateur | Ituri | Kasaï | Kasaï Mashariki | Katanga Juu | Kinshasa | Kivu Kaskazini | Kivu Kusini | Kongo Kati | Kwango | Kwilu | Lomami | Lomami Juu | Lualaba | Lulua | Mai-Ndombe | Maniema | Mongala | Sankuru | Tanganyika | Tshopo | Tshuapa | Ubangi Kaskazini | Ubangi Kusini | Wele Chini | Wele Juu
+/-