Mkalatusi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mkalatusi
(Eucalyptus spp.)
Muringamu au mti-mbao (Eucalyptus saligna)
Muringamu au mti-mbao (Eucalyptus saligna)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Plantae (Mimea)
(bila tabaka): Angiospermae (Mimea inayotoa maua)
(bila tabaka): Eudicots (Mimea ambayo mche wao una majani mawili)
(bila tabaka): Rosids (Mimea kama mwaridi)
Oda: Myrtales (Mimea kama mkarafuu)
Familia: Myrtaceae (Mimea iliyo na mnasaba na mkarafuu)
Jenasi: Eucalyptus
L'Hér.
Ngazi za chini

Spishi takriban 700

Mikalatusi au mikalitusi (kwa Kiing. gum tree) ni miti na vichaka ya jenasi Eucalyptus katika familia Myrtaceae.

Miti hii kiasili inatokea Australia na maeneo jirani ya Australasia. Kuna spishi zaidi ya 700 katika jenasi hii. Spishi 15 pekee ziko nje ya Australia. Siku hizi zinapatikana kote duniani kwa sababu zimepandwa kote katika maeneo tropiki na nusutropiki pamoja na Amerika, Afrika, nchi kando la Mediteranea, Mashariki ya Kati, China na Uhindi. Spishi zilizo nyingi haziwezi kustawi katika maeneo penye jalidi (kama halijoto inashuka chini ya sentigredi 0) maana mikalatusi haziwezi kukauka wakati wa baridi na kama halijoto inashuka mno maji katika matawi na shina inaganda na kuharibu seli zake.

Spishi mbalimbali zimeenezwa duniani kutokana na tabia zao za kukua haraka na hivyo kuwa chanzo cha ubao, kuwa na mafuta ndani yake yenye manufaa mbalimbali na wezo wao wa kukausha kinamasi na hivyo kupunza hatari ya malaria. Hivyo kuna pia upinzani dhidi ya kupanda mikalatusi kwa sababu zinatumia maji mengi[1].

Ukubwa na makazi[hariri | hariri chanzo]

Mikalatusi inapatikana kama vichaka au miti mikubwa hata mikubwa sana.

Mikalatusi za msituni huwa na shina moja ndefu na kilele cha matawi kisicho kirefu sana. Mkalatusi jitu (Eucalyptus regnans) ni mti wa majani mrefu kabisa; mmoja ulipatikana huko Tasmania mwenye urefu wa mita 97 na mzingo wa mita 20.

Vichaka vya mikalatusi vinafikia kimo cha chini ya mita 10.

Kimo cha miti yao hupangwa kuwa

  • midogo — hadimita 10
  • wastani — mita 10–30
  • mirefu — mita 30–60
  • mirefu sana - mita zaidi ya 60

Majani[hariri | hariri chanzo]

Karibu spishi zote huwa na majani mwaka wote lakini chache zinatupa majani wakati wa kiangazi. Kama spishi nyingi za familia ya myrtaceae majani huwa na tezi za mafuta.

Hata miti mikubwa mara nyingi hutoa kivuli kidogo tu kwa sababu majani yanatazama chini kwa kusudi la kupunguza athira ya nuru ya jua kwenye kanda la tropiki.

Majani mapya na majani yenye umri mrefu zaidi mara nyingi huonekana tofauti kwa rangi na umbo.

Ganda la miti[hariri | hariri chanzo]

Ganda inaonekana kulingana na umri wa mti. Kama miti yote mkalatusi unaongeza tabaka mpya ya ganda kila mwaka na hivyo kuongeza unene wa shina.

Kwenye spishi mbalimbali tabaka ya nje ya ganda inakauka na kuachana na shina kwa kanda ndefu au kwa vipande-vipande. Spishi nyingine zinashika ganda lililokauka kwenye sehemu ya chini ya shina pekee (kwa Kiingereza inaitwa "black butts" au "half bark"), sehemu ya juu ya shina huwa na ganda nyororo.

Mikalatusi na moto[hariri | hariri chanzo]

Mikalatusi huwa na aina ya mafuta ndani ya majani na ubao yanayoweza kuwaka. Kuna taarifa ya kwamba miti ililipuka wakati wa moto ya msituni. Moto zinaweza kuenea haraka kwenye misitu ya mikalatusi kwa sababu ndimi za moto zinaruka katika vilele vya matawi; katika hali ya joto mafuta kwenye majani huyeyuka kuwa mvuke ambako moto inaenea haraka mno. Miti ya mikalatusi zinaweza kudumisha moto kwa sababu baaada ya kuangamizwa nje kuna sehemu za kuotesha majanai na matwi zinzofichwa ndani ya ganda au kwenye sehemu ya mizizi yao. Pia mbegu ni ngumu haiharibiki haraka na kuota baada ya moto kupita.

Picha[hariri | hariri chanzo]

  1. "Santos, The Eucalyptus of California Section Three: Problems, Cares, Economics, and Species". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2013-09-28. Iliwekwa mnamo 2015-04-26.