Mimba za utotoni

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mimba za utotoni ni mimba kwa mwanamke aliye chini ya umri usiofaa kupata ujauzito katika jamii fulani.

Umri huo ni wa miaka 20, kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo linapenda kuchelewesha na kupunguza uzazi kwa jumla.[1] Mnamo 2015, takribani wanawake 47 kati ya 1,000 walikuwa na watoto chini ya umri huo, huku wengine milioni 3.9 walikuwa wametoa mimba. Mara nyingi hutokea zaidi vijijini kuliko mijini.

Mimba inaweza kutokea kwa kujamiiana baada ya kuanza kwa urutubishwaji wa yai la mwanamke, ambapo inaweza kuwa kabla ya hedhi ya kwanza lakini kwa kawaida hutokea baada ya mwanzo wa hedhi.[2] Kwa wasichana walio na lishe bora, hedhi ya kwanza hufanyika karibu na umri wa miaka 12 au 13.[3]

Athari za kiafya[hariri | hariri chanzo]

Wasichana wajawazito wanakabiliwa na masuala mengi yanayohusiana na ujauzito kama wanawake wengine wote.

Kuna wasiwasi wa ziada kwa wale walio chini ya umri wa miaka 15 kwani wana uwezekano mdogo wa kuwa na maendeleo ya kimwili ili kuendeleza mimba yenye afya au kuzaa.[4] Athari kama uzito mdogo wa kujifungua na upungufu wa damu zinaambatana na umri wa kibiolojia, kwani huzingatiwa wakati wa kujifungua hata baada ya kukidhi sababu nyingine kama vile ufikiaji wa utunzaji wa kabla ya kujifungua.[5][6]

Kumbe kwa wasichana wenye umri wa miaka 15-19, hatari huhusishwa zaidi na sababu za kijamii na za kiuchumi kuliko athari za kibiolojia kulingana na umri wao[7], ingawa ulimwenguni kote, matatizo yanayohusiana na ujauzito ndiyo yanayosababisha vifo vingi miongoni mwa wanawake wenye umri huo.

Sababu na uzuizi[hariri | hariri chanzo]

Mimba za utotoni zinahusishwa na masuala ya kijamii, ikiwa ni pamoja na viwango vya chini vya elimu na umaskini.

Mimba za utotoni katika nchi zilizoendelea kwa kawaida huwa nje ya ndoa na mara nyingi huhusishwa na maadili mabovu na unyanyapaa wa kijamii[8]. Katika nchi hizo takribani wanawake milioni 2.5 walio chini ya umri wa miaka 16 na wanawake milioni 16 wenye umri wa miaka 15 hadi 19 hupata watoto kila mwaka.

Mimba za utotoni katika nchi zinazoendelea mara nyingi hutokea ndani ya ndoa na karibu nusu yake huwa zimepangwa. Hata hivyo, katika jamii hizo, mimba zinaweza kuambatana na utapiamlo na huduma duni za afya na kusababisha matatizo ya kiafya [9][10].

Utamaduni[hariri | hariri chanzo]

Viwango vya mimba za utotoni ni vya juu zaidi katika jamii ambazo ni desturi kwa wasichana kuolewa wakiwa na umri mdogo ambapo wanahimizwa kuzaa watoto mara tu wanapofika wakati wa kushika ujauzito. Kwa mfano, katika baadhi ya nchi za Afrika, Kusini kwa Jangwa la Sahara, mimba za utotoni mara nyingi hutazamwa kama baraka kwa sababu ni uthibitisho wa uwezo wa kuzaa kwa mwanamke husika. Nchi ambazo ndoa za utotoni ni kawaida hupata viwango vya juu vya mimba za utotoni. Katika nchi ya India, ndoa za utotoni na mimba ni kawaida zaidi katika jamii za jadi za vijijini kuliko mijini.

Vijana wengi hawafundishwi maadili kuhusu jinsia wale mbinu za kudhibiti uzazi na jinsi ya kushughulika na watu wanaowashinikiza kufanya ngono kabla ya kuwa tayari. Vijana wengi wanaojamiiana hawana ukomavu wala utambuzi wa kutosha.[11]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Adolescent Pregnancy. World Health Organization. 2004. uk. 5. ISBN 978-9241591454. Iliwekwa mnamo 28 July 2017.  Check date values in: |accessdate= (help)
 2. "Can a Girl Get Pregnant if She Has Never Had Her Period?". 
 3. "Medscape: Medscape Access". 
 4. Mayor S (2004). "Pregnancy and childbirth are leading causes of death in teenage girls in developing countries". BMJ 328 (7449): 1152. PMC 411126. PMID 15142897. doi:10.1136/bmj.328.7449.1152-a. 
 5. "Poor obstetric performance of teenagers: Is it age- or quality of care-related?". Journal of Obstetrics & Gynaecology 24 (4): 395–398. 2004. PMID 15203579. doi:10.1080/01443610410001685529.  Unknown parameter |vauthors= ignored (help); Unknown parameter |s2cid= ignored (help)
 6. Abalkhail BA (1995). "Adolescent pregnancy: Are there biological barriers for pregnancy outcomes?". The Journal of the Egyptian Public Health Association 70 (5–6): 609–625. PMID 17214178. 
 7. Makinson C (1985). "The health consequences of teenage fertility". Family Planning Perspectives 17 (3): 132–139. JSTOR 2135024. PMID 2431924. doi:10.2307/2135024. 
 8. "Young mothers face stigma and abuse, say charities", BBC News, 2014-02-25. 
 9. Oringanje, Chioma; Meremikwu, Martin M; Eko, Hokehe; Esu, Ekpereonne; Meremikwu, Anne; Ehiri, John E (3 February 2016). "Interventions for preventing unintended pregnancies among adolescents". Cochrane Database of Systematic Reviews (kwa Kiingereza) 2016 (2): CD005215. PMC 8730506 Check |pmc= value (help). PMID 26839116. doi:10.1002/14651858.cd005215.pub3.  Check date values in: |date= (help)
 10. International technical guidance on sexuality education: An evidence-informed approach. Paris: UNESCO. 2018. uk. 18. ISBN 978-92-3-100259-5. 
 11. MacLeod, C. (1999). "The 'Causes' of Teenage Pregnancy: Review of South African Research – Part 2". South African Journal of Psychology 29: 8–16. doi:10.1177/008124639902900102.  Unknown parameter |s2cid= ignored (help)
Makala hii kuhusu mambo ya biolojia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mimba za utotoni kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.