Mauzo dijitali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mauzo dijitali (kwa Kiingereza "digital marketing") ni mbinu ya kutangaza biashara na kutafuta wateja inayoegemea matumizi ya mtandao. Huwa pia inahusu mauzo kwa kutumia simu za rununu, talakilishi au vifaa vingine vya kidijiti[1]

Ukuaji wake katika miaka ya 1990 na 2000 kwa sababu ya mapinduzi ya teknolojia ya intaneti ulibadilisha jinsi chapa na biashara zinavyotumia teknolojia kufanya mauzo. Mbinu za mauzo dijitali zimeenea kutokana na kuongezeka kwa wingi kwa watu wanaotumia vifaa vya kidijitali na kujumuishwa kwa majukwaa ya kidijitali katika mipango ya ununuzi na maisha ya kila siku [2] [3]. Mbinu za mauzo dijitali ni kama uimarishaji wa mashine za kutafuta tovuti (kwa Kiingereza "search engine optimization"), mauzo mashine za kutafuta tovuti (kwa Kiingereza "search engine marketing"), mauzo maudhui, mauzo waraghbishi, mauzo yanayoendeshwa na data, mauzo ya mitandao ya kijamii, uboreshaji wa mitandao ya kijamii na mauzo barua pepe. Njia nyingine ni pamoja na kutumia mbinu ya mauzo shirikishi. [4]

Historia ya mauzo dijitali[hariri | hariri chanzo]

Maendeleo ya mauzo dijitali hayatenganishwi na maendeleo ya teknolojia. Moja ya matukio muhimu yalitokea mwaka wa 1971, wakati Ray Tomlinson alipotuma barua pepe ya kwanza, na kuboreshwa kwa teknolojia yake kuruhusu watu kutuma na kupokea faili kupitia mtandao wa intaneti.[5]

Mwaka 1990 programu ya kwanza ya utafutaji kwa mtandao iliyojulikana kama "Archie search engine" ilianzishwa. Baadaye wachuuzi wengi walianza kuwa na wavuti zao binafsi na pia za biashara zao ambazo ziliwawezesha kufuatilia taarifa za wateja kwa ufanisi zaidi na kuwasiliana nao kwa urahisi.

Katika miaka ya 1990, neno mauzo dijitali lilibuniwa kwa mara ya kwanza.[6] Mwaka 1994 tangazo la mtandao lilitengenezwa na kampuni ya AT&T na katika kipindi cha miezi minne ya kwanza asilimia arubaini na nne ya walioona tangazo hili walilibofya.[7]

Katika miaka ya 2000, kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watumiaji wa intaneti na kuongezeka kwa watumiaji wa simu za mkononi, wateja walianza kutafuta bidhaa na kufanya maamuzi kuhusu mahitaji yao mtandaoni kwanza.

Mnamo mwaka wa 2007 ilitengenezwa teknolojia ya kufanya uuzaji uwe mara moja hata bila ya mchuuzi kuwepo katika mtandao wakati wa uchuuzi. Uendeshaji otomatiki wa mauzo ni mfumo ambao programu hutumika kuelekeza michakato ya kawaida ya mauzo. Uendeshaji otomatiki wa mauzo ulisaidia makampuni kugawa wateja katika makundi tofauti na kutoa maelezo ya kibinafsi kwa wateja, kulingana na shughuli zao mahususi.

Kuanzishwa kwa mitandao ya kijamii katika miaka ya 2000, kama vile LinkedIn, Facebook, YouTube na Twitter kumefanya watu wengi kutegemea sana vifaa vya kidijiti katika maisha ya kila siku. Mabadiliko ya tabia ya mteja yaliboresha mbinu za teknolojia ya mauzo. [8]

Mauzo dijitali leo[hariri | hariri chanzo]

Hivi leo mauzo dijitali yameendelea kuboreka na kumekuwa na watu wengi wanaouza vitu vyao katika mitandao. Kwa mfano, katika jumuia ya Afrika Mashariki, kuna wavuti kama Jumia, Kilimall na ulimwenguni kuna Amazon, eBay, Alibaba ambazo zinajulikana na watu wengi sana.

Pia kuna makampuni ambayo yanawasaidia wenye biashara kuuza kidijitali na pia wanunuzi kujua mbinu mbalimbali za kufaidika na mauzo dijitali.

Uhamasishaji wa Chapa[hariri | hariri chanzo]

Mojawapo ya malengo muhimu ya mauzo dijitali ni kuongeza ufahamu wa chapa kwa kiwango ambacho wateja na umma kwa ujumla wanaifahamu na kuitambua chapa fulani.

Kuimarisha ufahamu wa chapa ni muhimu katika mauzo dijitali, na mauzo kwa ujumla, kwa sababu ya athari zake kwenye mtazamo kuhusu chapa na ufanyaji maamuzi wa wateja.[9]

Mbinu za mtandaoni zinazotumika kujenga ufahamu wa chapa[hariri | hariri chanzo]

Mikakati ya mauzo dijitali inaweza kujumuisha utumiaji wa njia na mbinu moja au zaidi za mtandaoni ili kuongeza ufahamu wa chapa miongoni mwa watumiaji wake. Kujenga ufahamu wa chapa kunaweza kuhusisha mbinu/zana kama vile:

Uimarishaji wa mashine ya utafutaji tovuti (SEO)[hariri | hariri chanzo]

Mbinu za kuimarisha mashine za utafutaji tovuti zinaweza kutumika kuboresha mwonekano wa tovuti za biashara na maudhui yanayohusiana na chapa ili zisomewa kwa urahisi na programu za utafutaji kama Google, Bing na Yahoo.[10]

Katika mbinu hii, mwenye wavuti huhakikisha kwamba watafutaji waona wavuti yake ukurasa wa kwanza wanapotafuta katika programu za kutafuta. Hili hufanywa kwa kutafuta nukuu katika wavuti nyingine pamoja na kuandika makala yenye mada anayotafuta mtafutaji. Hivi leo wanaodhibiti Google wasema kwamba ni muhimu mwenye wavuti ahakikishe kwamba wavuti wake unajibu maswali anayotafuta mtafiti.[11]

OFF Ukurasa SEO[hariri | hariri chanzo]

Uuzaji wa Mitandao ya Kijamii: Kujihusisha na hadhira yako kwenye majukwaa mbalimbali ya mitandao ya kijamii, kushiriki maudhui muhimu, na kujenga uwepo thabiti wa mitandao ya kijamii kunaweza kuathiri vyema mwonekano wa tovuti yako na ufahamu wa chapa yako.

 • Uuzaji wa Ushawishi: Kushirikiana na washawishi au wataalamu wa tasnia ili kukuza maudhui au bidhaa zako kunaweza kusaidia kupanua ufikiaji wako na kuvutia trafiki inayofaa zaidi kwenye tovuti yako.
 • Chapisho la Wageni: Kuandika maudhui ya ubora wa juu kwa tovuti nyingine zinazotambulika katika eneo lako la niche na kujumuisha kiungo cha kurudi kwenye tovuti yako kunaweza kusaidia kujenga mamlaka, kuendesha trafiki, na kuboresha viwango vya injini ya utafutaji.
 • Mitajo ya Biashara ya Mtandaoni na Biashara: Kuangaziwa katika machapisho ya mtandaoni, matoleo kwa vyombo vya habari, na kupata mitaji ya chapa kutoka kwa vyanzo halali kunaweza kuboresha sifa ya tovuti yako na kuongeza mwonekano wake.
 • SEO ya ndani: Ikiwa una uwepo wa kawaida, kuboresha tovuti yako kwa hoja za utafutaji wa ndani na kuorodheshwa kwenye saraka za biashara za karibu kunaweza kukusaidia kuvutia wateja zaidi wa ndani.
 • Uuzaji wa Video: Kuunda na kutangaza maudhui ya video yanayovutia kwenye majukwaa kama vile YouTube hakuwezi tu kuvutia hadhira tofauti bali pia kuboresha mwonekano wako wote mtandaoni.
 • Mijadala ya Mtandaoni na Tovuti za Maswali na Majibu: Kushiriki katika jumuiya husika za mtandaoni na kutoa majibu muhimu kwa maswali ya watumiaji kunaweza kuanzisha ujuzi wako na kurudisha trafiki kwenye tovuti yako.
 • Ushirikiano wa Biashara na Ushirikiano: Kushirikiana na biashara au tovuti nyingine katika sekta yako kwa juhudi za utangazaji-shirikishi kunaweza kusaidia kupanua ufikiaji wako na kuboresha uwepo wako mtandaoni.
 • Podikasti: Kushiriki katika podikasti au kuanzisha podikasti yako mwenyewe kunaweza kukusaidia kufikia hadhira mpya na kujiimarisha kama mamlaka katika uwanja wako.
 • Maoni na Ushuhuda Mtandaoni: Kuhimiza wateja walioridhika kuacha maoni na ushuhuda chanya kwenye majukwaa ya ukaguzi na tovuti yako inaweza kuboresha sifa na uaminifu wako mtandaoni.

Ni muhimu kukumbuka kuwa SEO ya nje ya ukurasa inapaswa kulenga kila wakati kutoa thamani kwa watumiaji na kujenga uhusiano wa kweli, badala ya kulenga tu kudhibiti viwango vya injini ya utafutaji. Mbinu za SEO za kofia nyeusi, kama vile kutumia zana za kiotomatiki za kuunda viungo (k.m., GSA, Money Robot), kuweka maneno muhimu, au kutoa maoni kwa barua taka, kunaweza kusababisha adhabu kali kutoka kwa injini za utafutaji na kudhuru mwonekano wa tovuti yako kwa muda mrefu.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. "Definition of digital marketing". Financial Times. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2017-11-29. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2015. {{cite web}}: More than one of |accessdate= na |access-date= specified (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
 2. Dahlen, Micael (2010). Marketing Communications: A Brand Narrative Approach. Chichester, West Sussex UK: John Wiley & Sons Ltd. uk. 36.
 3. Nielsen (20 Januari 2016). "Connected Commerce is Creating Buyers Without Border". Nielsen Global. Nielsen Global. Iliwekwa mnamo Machi 25, 2016.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 4. "Digital Marketing". Techopedia. Iliwekwa mnamo 22 Agosti 2015.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 5. hello_world. "First Network Email sent by Ray Tomlinson". www.computinghistory.co.uk. Iliwekwa mnamo 9 Machi 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 6. "Everyone Is Burned Out, But No One Knows What That Means", The End of Burnout, University of California Press, ku. 19–36, 2022-01-04, iliwekwa mnamo 2022-06-03
 7. Joe McCambley (2013-12-12). "The first ever banner ad: why did it work so well?". the Guardian (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-03.
 8. "Connected Commerce Is Creating Buyers Without Borders". Nielsen Global. Iliwekwa mnamo 6 Machi 2018.{{cite web}}: CS1 maint: date auto-translated (link)
 9. Chovanová, Henrieta Hrablik; Korshunov, Aleksander Ivanovich; Babčanová, Dagmar (2015-01-01). "Impact of Brand on Consumer Behavior". Procedia Economics and Finance. International Scientific Conference: Business Economics and Management (BEM2015) (kwa Kiingereza). 34: 615–621. doi:10.1016/S2212-5671(15)01676-7. ISSN 2212-5671.
 10. "How to Use SEO to Build Your Brand". Neil Patel (kwa Kiingereza). 2016-02-20. Iliwekwa mnamo 2022-06-03.
 11. 1 2k Shares, 35k Reads. "Why Your SEO Focus Should Be Brand Building". Search Engine Journal (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2022-06-03.{{cite web}}: CS1 maint: numeric names: authors list (link)
Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mauzo dijitali kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.