Matabeleland North

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Mkoa wa MAtabeleland North katika Zimbabwe

Matabeleland North ni mkoa wa Zimbabwe upande wa kaskazini ya Bulawayo. Kuna wakazi 700,000 (2005) katika eneo la kilomita za mraba 75,025 .

Makao makuu ya mkoa yapo mjini Lupane. Mkoa umepakana na Bulawayo, Matabeleland South, Midlands na Mashonaland West. Kuna mipaka ya kimataifa na Zambia upande wa kaskazini kwenye mto Zambezi na Botswana upande wa kusini-magharibi.

Miji mikubwa kidogo ni Hwangwe na Victoria Falls.

Mkoa unaweza kuvuta watalii hasa kwa maporomoko ya Victoria Falls na hifadhi ya taifa ya Hwangwe.

Utawala[hariri | hariri chanzo]

Matabeleland North kuna wilaya 7: