Marriane Fannin

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Marriane Fannin
Amekufa 18 Novemba 1938
Nchi Bendera ya Afrika Kusini Afrika Kusini
Kazi yake msanii wa uchoraji


Marianne au Edda Fannin (2 Machi 184518 Novemba 1938) alikuwa msanii wa mimea kutoka Ireland, anafahamika kwa kazi yake ya uchoraji wa mimea ya Afrika Kusini.[1] Alichukuliwa kama msanii nguzo wa usanii wa mimea Afrika kusini wa wakati wake.[2]

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Marianne Edwardine Fannin alizaliwa Dublin, akiwa mtoto wa Thomas and Ellen Fannin. Alipokuwa na umri wa miezi michache, familia yake ilihamia Afrika Kusini kutokea Dublin.[3] Awali waliishi katika rasi Capetown.[4]

Fannin aliolewa na mchungaji Eustace Wilberforce Jacob mwaka 1869. Wenza hao walisafiri hadi Uingereza mwaka 1871, ambapo Jacob alifariki muda mfupi baada ya kufika. Fannin alibaki Uingereza kwa muda akisomea muziki na uchoraji. Alirejea Afrika Kusini mwaka 1875.

Kutokea 1878, aliishi Afrika Kusini, Transavaal na kuolewa na mchungaji Alfred Roberts mnamo 1879 aliyekutana naye kupitia hafla ya kanisa. Robert aliendelea na kuwa shemasi wa Anglikana dayosisi ya Pretoria. Wenza hao waliishi Potchefstroom kutokea 1881 mpaka 1896, ambapo walijaliwa wavulana wawili. Fannin alikwua muasisi wa Shule ya wasichana ya St. Mary's Diocesan School for Girls, Pretoria na Robert alihudumu kama mwalimu mkuu wa shule ya wavulana St Birinus's.

Mnamo mwaka 1881, wakati wa uvamizi Pretoria, Fannin alirudi kwenye makazi ya familia yaliyoko Natal.[3] Fannin alifariki tarehe 18 Novemba 1938, akiwa kati ya Heidelberg, Gauteng[1][4] au akiwa Muckleneuk, Pretoria.[3]

Kazi ya sanaa[hariri | hariri chanzo]

Fannin alikua msanii wa kujifunza mwenyew. Alitiwa moyo na kaka yake mkubwa, George Fox Fannin mtaalamu hodari wa mimea aliyesomea mimea asili ya Afrika Kusini[3] Dhamira zao zilikua juu ya Orchidaceae|orchids na Asclepiadoideae (milkweeds).[4] Dhamira hii ilipelekea Fannin kuchora mimea ambayo George alikusanya na kuituma michoro hiyo kwa William Henry Harvey akiwa Trinity College, Dublin. Harvey alivutiwa sana na michoro ile na kulipa Orchid jina lake kwa heshima yake kama mgunduzi wake.[3] Mpaka 1869, Fannin alichora albamu ikionyesha maua ya Natal. Mnamk 1878 Fannin alikua mwanachama wa chama kanisa kilichoongozwa na Askofu Henry Bousfield, nabwakati wa safari yao kutokea Durban kwenda Pretoria Fannin alichora michoro mfano wa mazingira waliyopita. Wakati akiishi Transvaal, Fannin alichora maua pori na na mandhari.Michoro yake imehifadhiwa na shule ya mimea ya Trinity College, Dublin. Michoro yake ya mandhari imehifadhiwa katika makusanyo binafsi ya picha Afrika Kusini.[5]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Gunn, Mary; Codd, L. E. W. (1981). Botanical Exploration Southern Africa. CRC Press. ku. 152–153. ISBN 978-0-86961-129-6. 
  2. Harris, Mary N. (2007). Sights and Insights: Interactive Images of Europe and the Wider World. Pisa: Edizioni Plus. uk. 81. ISBN 978-88-8492-467-4. 
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 Butler, Patricia (2000). [[[:Kigezo:Google books]] Irish Botanical Illustrators & Flower Painters]. Suffolk: Antique Collectors' Club. ku. 112–113. ISBN 978-1-85149-357-9. 
  4. 4.0 4.1 4.2 Creese, Mary R. S.; Creese, Thomas M. (2010). [[[:Kigezo:Google books]] Ladies in the Laboratory]. Vol. III: South African, Australian, New Zealand, and Canadian Women in Science: Nineteenth and Early Twentieth Centuries. Plymouth: Scarecrow Press. ku. 7–8. ISBN 9780810872899. 
  5. Hitilafu ya kutaja: Invalid <ref> tag; no text was provided for refs named JSTOR
Makala hii kuhusu mtu huyo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Marriane Fannin kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.