Nenda kwa yaliyomo

Malengamakali

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Malenga Makali)


Kata ya Malengamakali
Nchi Tanzania
Mkoa Iringa
Wilaya Iringa Vijijini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 9,394

Malengamakali ni kata ya tarafa ya Ismani, Wilaya ya Iringa Vijijini katika Mkoa wa Iringa, Tanzania, yenye Postikodi namba 51218.

Vijiji vyake ni kama vileː Usolanga, Iguluba, Makadupa, Mkulula na Nyakavangala.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 9,394 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,917 waishio humo. [2] Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ilikuwa na wakazi wapatao 7,597 waishio humo. [3]

Ni eneo maarufu kwa kilimo hasa cha mahindi, ingawa ardhi imechoka kutokana na matumizi makubwa, hasa katika miaka ya 1950 na 1960, Ismani peke yake ilipokuwa inaweza kuzalisha kuliko Tanzania nzima.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo, hasa Wakatoliki na Walutheri.

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. Sensa ya 2012, Iringa Region- Iringa District Council
  3. "2002 Population and Housing Census General Report" (kwa Kiingereza). Government of Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-03-18. Iliwekwa mnamo 2008-08-21.
Kata za Wilaya ya Iringa Vijijini - Tanzania

Idodi | Ifunda | Ilolompya | Itunundu | Izazi | Kalenga | Kihanga | Kihorogota | Kising'a | Kiwere | Luhota | Lumuli | Lyamgungwe | Maboga | Magulilwa | Mahuninga | Malengamakali | Masaka | Mboliboli | Mgama | Migoli | Mlenge | Mlowa | Mseke | Nyang'oro | Nzihi | Ulanda | Wasa


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Iringa bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Malengamakali kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.